Sunday 2 April 2017

Shilole Ajivisha Pete ya Uchumba mwenyewe.Fahamu zaidi hapa.

STAA wa Filamu za Kibongo, Zuwena Mohammed ameamua kujivisha pete ya uchumba mwenyewe, kitendo ambacho kimezua minong’ono kwa watu wengi wakidai kuwa amevishwa na mtu ambaye hajamuweka wazi.

Akizungumza na Ijumaa, Shilole alisema kuwa aliwahi kuvishwa pete na aliyekuwa mpenzi wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, ikapotea kitatanishi kisha Nuh akaoa mwanamke mwingine hivyo akaona kuliko kidole hicho kibaki tupu, akisitiri.

“Pete ile ya Nuh ilipotea, sijui huwa ni za mashetani? Nimeona ninunue nyingine niivae, hakuna cha mwanaume wala nini, mimi sijaona tatizo kuivaa na huenda ndiyo naiita ndoa,” alisema Shilole.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment