Mkazi wa Buguruni jijini hapa, Deus Johakim Magosa (45) ambaye ni
shahidi wa nane upande wa Jamhuri katika kesi namba 303 ya mwaka 2016 ya
kumjeruhi, kumtoboa macho na kumfanyia unyang’anyi wa kutumia silaha,
Saidi Mrisho inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ katika Mahakama ya
Wilaya ya Ilala jijini, leo alinusurika kutupwa lupango baada ya Wakili
Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga kumtuhumu kutoa ushahidi wa
uongo.
Wakili Katuga alimtuhumu shahidi huyo kutokana na kutoa majibu tofauti
wakati akimuongoza kutoa ushahidi wake na maelezo aliyoyatoa awali Kituo
cha Polisi cha Buguruni.
Awali shahidi huyo alisema mahakamani hapo kuwa hakuwahi kusikia popote
kuwa Scorpion amehusishwa katika tukio la kumshambulia Said, lakini
baadaye alipobanwa alisema ni kweli alisikia tetesi hizo kuwa mtuhumiwa
huyo ndiye aliyefanya tukio hilo. Pamoja na mambo mengine aliyomhoji na
kumbaini kuwa anatoa ushahidi wa uongo wakili Katuga
alipomgeukia hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Flora Haule na
kumwambia shahidi anazidi kuidanganya mahakama hiyo na kuitaka mahakama
hiyo imchukulie hatua kwa mujibu wa kifungu cha 164 cha ushahidi hapa
nchini (Tanzania Evidence Act).
Shahidi huyo alionekana kuwa katika wakati mgumu baada ya wakili huyo
kuwaita askari polisi na kuwataka wakae tayari kumchukua shahidi huyo.
Hata hivyo kutokana na ufinyu wa muda hakimu Flora aliahirisha kesi hiyo
mpaka Aprili 18 mwaka huu na kumuacha shahidi huyo aondoke na kumtaka
kufika tena mahakamani hapo tarehe iliyopangwa bila kukosa ambapo
Scorpion naye alirudishwa mahabusu mpaka tarehe hiyo.
Mwandishi wetu alizungumza na mmoja wa wanasheria mahakamani hapo kuhusu
ushahidi wa uongo ambapo, mwanasheria huyo alisema unapobainika kutoa
ushahidi wa uongo ukiwa ndani ya kiapo unaweza kufungwa jela kati ya
miezi sita mpaka mwaka mmoja.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment