Moja ya makala zilizopita niliwahi kuongelea namna ya kupata mtoto wa
kiume na jinsi ya kujua siku za mwanamke za hatari za kubeba mimba ni
zipi lakini watu wengi wamekua wakinipigia simu kwamba hawakuelewa.
Siku za hatari za mwanamke ni zipi?
Hizi ni siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata
ujauzito bila wasiwasi wowote labda kama ana matatizo yanayomfanya
asibebe mimba au mwanaume wake ana matatizo.
Utazijuaje siku hizo?
Kwanza kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za
mzunguko wako. Kuna aina tatu za mzunguko.. mzunguko mrefu ambao
unachukua siku 35, mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida
unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao.
Unajuaje mzunguko wako?
Hesabu siku tangu siku ile ya kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka
siku moja kabla ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata. Unashauriwa
uchukue miezi mitatu mpaka sita ukihesabu ili ue na uhakika kwamba
mzunguko wa tarehe zako haubadiliki, kama umeshahesabu siku za nyuma
kabla ya kusoma makala hii ni vizuri pia. Mfano umeanza kuona siku zako
tarehe moja mwezi wa nne alafu ziko zako zingine ukaziona tarehe 29
mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata 28.. maana yake wewe unamzunguko
wa siku 28.
Je siku za hatari ni zipi?
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku
ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi
wanachanganya na kupata mimba.
Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku 28, chukua 28 toa 14
utapata 14. Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua
mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza
kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla na
siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari hivyo siku za hatari ni ni siku
ya 10,11,12,13,14 na 15.
Kama mzunguko wako ni mrefu labda siku 36 basi chukua 36 toa 14 utapata
22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.
Kama mzunguko wako ni mfupi, mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua
21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni siku yai linashuka hivyo ni
hatari kwa huyu mtu.hivyo siku zingine za hatari ni 3,4,5,6,7[mtoto wa
kiume] na 8.
kama mzunguko wako ni wa kawaida yaani siku 28 sasa chukua 28 toa 14
unapata 14 yaani siku ya 14 ndio hatari zingine ni siku ya
10,11,12,13,14,15
Dalili kwamba uko kwenye siku za hatari ni zipi?
Kuongezeka kwa joto kidogo, tumbo kuuma kidogo, na ute mweupe kutoka sehemu za siri..
mwisho: maelezo hayo hapo juu yanaweza kusaidia kupanga uzazi,
kuchagua jinsia ya mtoto au kutafuta mtoto. Lakini pia tarehe zote
nilizoweka mabano ambazo ndio tarehe yai linashuka ndio za mtoto wa
kiume zingine zote zilizobaki ni za watoto wa kike. kwa lugha ya
kingereza soma hapa
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment