KUFUATIA madai kuwa, mrembo mwenye figa matata Bongo, Agnes Gerald
‘Masogange’ anaishi na kigogo mmoja kwenye mjengo wa kifahari kule
Makongo Juu jijini Dar na yale madai kuwa, anatumia madawa ya kulevya,
kikosi kazi cha Operesheni Fichua Maovu cha Global (OFM), kiliamua
kumvaa kininja nyumbani kwake.
MADAI KWANZA
Madai ya mwanzo yaliyotua kwenye dawati la IJUMAA yalikuwa ni kwamba,
eti modo huyo hufika nyumbani hapo mida ya usiku akiwa na mwanaume huyo
ambaye hakuweza kufahamika kama ni yule Dick Sound aliyetajwa kutoka
naye awali au ni mwingine. Aidha, kutokana na mrembo huyo kutopatikana
kirahisi kwenye simu yake ya mkononi, gazeti hili likiwa na lengo pia la
kutaka kuonana naye ana kwa ana kuzungumzia mambo mbalimbali ya
kimaisha sambamba na mwenendo wa kesi yake ya madawa ya kulevya,
liliamua kumfuata nyumbani kwake.
DAY 1 OFM KAZINI
Jumatatu, Machi 27, majira ya saa 12 jioni, OFM walifika nyumbani kwa
Masogange na kugonga geti bila kufunguliwa hivyo wakakaa nje hadi saa 3
usiku lakini hakuonekana mtu yeyote kuingia wala kutoka.
DAY 2 OFM KAZINI
Mapema alfajiri ya siku iliyofuata Machi 28, makachero hao wa OFM
walidamkia nyumbani hapo ambapo kuanzia saa 12 mpaka saa 1 usiku hakuna
mtu aliyetoka wala kuingia.
OFM WAZAMA NDANI
Baada ya kuona kimya, OFM waliamua kusogea mpaka getini na kugonga
lakini kwa muda wa dakika kumi walizogonga, hawakuweza kufunguliwa ndipo
walipoamua kuingia ‘kininja’ kupitia kigeti kidogo ambacho hakikuwa
kimefungwa.
Baada ya kuingia ndani na kubisha mlango wa nyumba anayoishi Masogange,
alitokea msichana aliyejitambulisha kama mdogo wake na baada ya salamu
mazungumzo yalikuwa hivi; OFM: Tuna shida na Masogange, tunataka kuongea
naye mambo ya kisanii.
Binti: Mh! Dada hayupo, ila ngoja nizungumze na dada yake halafu nawapa
jibu… (anaingia ndani kisha muda mfupi anarudi na kuwakaribisha OFM
ndani).
Muda mfupi baada ya OFM kuingia ndani, anakuja mwanadada mrembo mwenye
figa kama ya Masogange na kujitambulisha kuwa ni dada yake na kuwauliza
OFM walikuwa na shida gani.
OFM: (kwa kuzuga) Sisi ni wasanii, tumekuja hapa kwa ajili ya kazi,
tunayo ngoma yetu ambayo tunataka Masogange ashiriki kwenye video.
DADA MTU: Kwanza nani kawadairekti kuwa Masogange anaishi hapa?
OFM: Sisi ni wakazi wa maeneo haya.
DADA MTU: Oke, sasa ipo hivi Masogange hayupo, lakini pia hashiriki tena
kwenye video, kwani nyie mmemuona mara ya mwisho lini? Si muda umepita?
Ndiyo hivyo sasa tafuteni mtu mwingine.
OFM: Kwa nini hafanyi muziki?
DADA MTU: Hilo ni suala binafsi siwezi kulijibu, nafikiri tumemaliza, naomba muondoke.
Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, OFM walisikia sauti ya watu kutokea
chumba kingine, hali iliyowafanya wahisi ni Masogange na mtu mwingine.
Hata hivyo, kufuatia dada mtu huyo kuamuru OFM waondoke, zilikuwa
zimebainika siri nzito za maisha yake ikiwa ni pamoja na kuishi kifahari
kutokana na mandhari ya sebuleni ilivyo.
Pili, mbali na dada yake wapo wadada wawili wa kazi na kubwa zaidi ni
kwamba, ule mjumba unaotajwa kuwa kapangishiwa, haishi peke yake bali
kuna wapangaji wengine hivyo wale wanaodhani anaishi kwenye bonge la
mjumba, mawazo hayo yafutike.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment