Na Daudi Manongi - MAELEZO
Serikali
kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesaini msaada wa shilingi Bilioni
490 usiokuwa na masharti yeyote kutoka Umoja wa Ulaya ikiwa ni msaada wa
kibajeti kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka wa bajeti wa
2017/18.
Mkataba
huo umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto
James kwa niaba ya Serikali na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini
Bw.Roeland van de Geer kwa niaba ya Umoja wa Ulaya.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba huo Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amesema Umoja wa Ulaya umetoa
msaada huo kutokana na kuvutiwa na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano
katika maeneo mbalimbali ikiwemo kupambana na rushwa na ubadhirifu wa
mali za umma.
“Nadhani
mmeshuhudia utiaji saini huu ulioisha hivi punde na Umoja wa Ulaya
wametuhakikishia kuendelea kutusaidia katika masuala ya misaada ya
kibajeti pamoja na kuwa bega kwa bega na Serikali katika masuala
mbalimbali ya maendeleo”, aliongeza Katibu Mkuu huyo.
Pamoja
na hayo mpango wa pili wa maendeleo wa Taifa wa Bajeti ya mwaka 2017/18
pia utapewa msaada na umoja huo kwani wameuona mpango huo una tija na
kuweka mkazo katika viwanda na kilimo.
Kwa
upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Roeland Van de Geer
amesema kuwa wameliangalia zaidi suala la utawala kama eneo kuu katika
mpango wa ushirikiano na Tanzania na vilevile wanatazamia maendeleo
zaidi katika maeneo ya kilimo,ujenzi wa barabara za vijijini na nishati.
“Mkataba
ambao tumeusaini utaiwezesha Wizara ya Fedha na Mipango katika
ukusanyaji wa mapato,zitaboresha uwajibikaji na utumiaji mzuri wa mali
za Serikali, na Umoja wa Ulaya unasapoti azma ya viwanda ya Serikali ya
Awamu ya Tano,”Aliongeza Roeland Van de Geer.
Amesema
kuwa ushirikiano uliopo katika ya Tanzia na Umoja wa Ulaya ni mpana
sana na utaendelea kuimarika zaidi katika kipindi hiki ambacho mageuzi
ya sera yanahitajika.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment