Monday 3 April 2017

Mbwana Samatta apanda thamani.Fahamu zaidi hapa.

Thamani ya Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta imepanda katika soko la wachezaji duniani.

Thamani yake kwa imefikia kiwango cha Euro milioni 3 sawa na shilingi bilioni 7.1 za kitanzania kwa mujibu wa mtandao unaohusika na biashara za wachezaji duniani.

Hatua hiyo imekuja baada ya Samatta kutimiza idadi ya kiwango cha magoli iliyokuwa ikihitajika ambapo ameweza kufunga mabao saba katika mechi sita za hivi karibuni akiwa katika timu yake ya Genk pamoja na mawili aliyoyapachika Botswana mchezo uliochezwa na Taifa Stars

Mabadiliko hayo yamefanyika mwishoni mwa mwezi Machi ambapo mshambuliaji huyo alionekana kung’ara katika ushindi wa bao 4-1 iliyopata klabu yake dhidi ya Lokeren na yeye akitupia bao mojawapo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment