Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri majini na nchi na kavu (SUMATRA)
Gilliard Ngewe amesema huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo nchini
zitaendelea kama kawaida hapo kesho baada ya wamiliki wa vyombo vya
usafiri nchini kuzungumza na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame Mbarawa.
Makubaliano hayo yalifikiwa mapema leo baada ya wamiliki wa mabasi
(TABOA), wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UWADAR) pamoja na wamiliki
wamalori(Tatoa) kuzungumza na Profesa Mbarawa na kukubaliana kubadili
kanuni na kuzitafsiri kwa lugha ya Kiswahili.
Walikubaliana kuzifanyia marekebisho kanuni hizo ndani ya siku 14 na
zipelekwe kwa wadau, pia zitenganishe makosa ya madereva na makosa ya
wamiliki.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment