MKWASA
Inadaiwa
 Mkwasa anaidai TFF mshahara wa zaidi ya miezi miwili ambapo kwa mwezi 
anapokea kiasi cha shilingi milioni 28 mshahara aliourithi kwa aliyekuwa
 kocha wa timu hiyo, Martin Nooij ambaye naye aliurithi kutoka kwa 
Mbrazili, Marcio Maximo ambao walikuwa wakilipwa na serikali ya awamu ya
 nne, hivyo kulifanya sasa shirikisho hilo kuwa na mzigo mkubwa katika 
suala zima la kulipa mshahara huo.
Hivi karibuni Malinzi alikiri juu ya kudaiwa mshahara na Mkwasa ambapo aliahidi kutekeleza jukumu hilo ndani ya mwezi huu.
Taarifa
 kutoka ndani ya shirikisho hilo imeelezwa kuwa, mshahara wa Mkwasa 
umekuwa mzigo mkubwa TFF kutokana na ukubwa wake na kuwa uongozi wa juu 
unahaha kulipa.
“Hakukuwa na mazungumzo ya makubaliano tangu awali juu ya Mkwasa kurithi mshahara huo.
“Baada
 ya kuja Mkwasa kuna waziri aliamua kuuhamishia mshahara huo kwa kocha 
huyo bila ya kuwepo kwa mazungumzo ya makubaliano na TFF, hivyo kujikuta
 wakitakiwa kumlipa kiasi hichohicho jambo ambalo ni mzigo mkubwa 
kutokana na kiasi cha fedha kuwa kikubwa kwa kuwa serikali hailipi 
mshahara huo kama ilivyokuwa awali.
“Unajua
 mshahara anaolipwa Mkwasa unaweza kulipa nusu ya wafanyakazi wote 
waliopo TFF, hivyo unaona ni jinsi gani hali ilivyokuwa ngumu, hata sasa
 hajalipwa kwa miezi miwili iliyopita, huu tunaenda mwezi wa kumi, 
lakini kuna utaratibu unaoendelea ili aweze kulipwa fedha zake zote 
ndani ya mwezi huu.
“Mkwasa
 anatarajia kumaliza mkataba wake Machi, mwakani, naamini itabidi 
wamlipe tu hadi utakapofikia tamati na baada ya hapo haijajulikana kama 
ataongezewa mwingine ama la,” kilisema chanzo.
Aidha ilielezwa kuwa hata wafanyakazi wa TFF nao hawajalipwa kwa miezi miwili lakini wanatarajiwa kulipwa mwezi huu.
Alipotafutwa
 Msemaji wa TFF, Alfred Lucas kuhusu suala hilo alisema yupo kwenye 
kikao atafutwe baadaye, alipotafutwa baadaye hakupatikana hewani. 
Alipotafutwa Mkwasa kuzungumzia hilo, hakupokea simu.
SOURCE: CHAMPIONI
 








 




 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment