Home »
Makala
» UKIZIONA DALILI HIZI JUA PENZI LIMEINGIA DOA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Hisia zinakuwa na nafasi kubwa sana kwa
mwanamke, kwani mwanamke huishi kwa hisia zaidi kuliko mwanaume,
Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya dalili zinazoweza kuonyeshwa na
mwanamke ambaye anatoka au yupo kwenye harakati za kutoka nje ya ndoa
yake.
1.KUCHELEWA:
Kuna wakati mwanamke anaweza kuaga kwamba anakwenda saluni au kusuka,
badala ya kurejea kwa muda ambao umezoeleka, anachukua muda mrefu hata
mara tatu zaidi.
2.KUBADILI MAENEO:
Hebu chukulia kwamba, mwanamke amezoea kwenda soko fulani la karibu,
hospitali fulani ya karibu, saluni fulani ya karibu na hata nyumba
fulani ya ibada ya karibu. Unapoona anahama maeneo ya karibu ya huduma
na kwenda ya mbali, bila sababu ya msingi, huna budi kuanza kutuhumu
mwenendo mbaya.
Siyo lazima kuhama kokote kuwe na
mwenendo mbaya, lakini kama kuhama kwenyewe kunatia shaka kwa sababu
maelezo ya kuhama huko hayana msingi, mwanaume ana kila sababu ya
kuchunguza kama hakuna usaliti unao anywa.
3.UNUNUZI USIO WA KAWAIDA:
Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake kwa ajili ya kupata fedha, basi
atakuwa na mabadiliko makubwa katika mtindo wake wa manunuzi.Atakuwa
ananunua vitu vya thamani kubwa kuliko uwezo wake, atakuwa na fedha
nyingi tofauti na ambazo angekuwa nazo na pengine kumiliki mali kama
nyumba kwa siri.
4.KUANZISHA VURUGU:
Kuna wakati mwanamke anayetoka nje ya ndoa huanzisha vurugu za makusudi
na mumewe. Lengo la kuanzisha vurugu hizo ni ili apate nafasi ya
kujifanya amezira na kuondoka nyumbani kwa muda. Huo muda anapoondoka
nyumbani kujifanya kakerwa na vurugu hizo ndiyo muda ambao anautumia
kwenda kwa mchepuko wake.
5.KUSITISHA UAMINIFU:
Mwanamke anayetoka nje ya ndoa, mara nyingi husimamisha kumwamini
mumewe, yaani hayuko tayari kushiriki masuala ya siri, ambayo wanandoa
huwa wanashiriki. Husita kumshirikisha mumewe kwenye mambo yake mengi.
Lakini pia husita kumuomba mumewe ushauri, kama alivyokuwa akifanya siku
za nyuma.
6.KUACHA KUVAA PETE:
Kuna sababu nyingi ni kwa nini mwanamke anaweza kuacha kuvaa pete yake
ya ndoa. Moja ya sababu hizo ni kusalitiwa na mumewe au ndoa yake kuwa
kwenye misukosuko mikubwa sana. Lakini nje ya misukosuko mikubwa ya
ndoa, sababu nyingine inayoweza kumpelekea mwanamke kuvua mara kwa mara
au moja kwa moja pete yake ya ndoa, ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa
yake.
0 comments:
Post a Comment