Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahimu Akilimali
ametangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa klabu ya hiyo iliyoachwa wazi
hivi karibuni na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.
Hivi karibuni Manji alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake hiyo
ili aweze kupumzika kutokana na matatizo mbalimbali aliyokumbana nayo
siku chache zilizopotia.
Lakini pia maamuzi hayo ya Manji yalikuja ikiwa ni muda mfupi tu
umepita tangu alipotangaza kutaka kuikodi timu hiyo kwa muda wa miaka
10, lakini akakukumbana na changamoto kibao kutoka kwa baadhi ya
wanachama wa klabu hiyo na kuamua kusitisha mpango wake huo.
Akilimali alisema anaamini amefikia uamuzi huo ili aweze kuleta
mabadiliko makubwa ya ndani ya klabu hiyo kuanzia pale Manji alipoishia.
Alisema licha ya kutokuwa bilionea kama ilivyokuwa kwa Manji lakini
anaamini kwa kutumia utajiri wake wa hekima na busara alizonazo
ataiongoza klabu hiyo kwa mafanikio makubwa, kwa hiyo amewataka
wanachama kutulia.
“Manji keshaondoka Yanga akapumzike kutokana na matatizo
yaliyompata hivi karibuni kwa hiyo siyo vizuri kuanza kuumiza vichwa
kuwa mambo yatakuaje bila ya yeye.
“Yanga ni timu kubwa, jina lake na nembo yake tu chanzo kikubwa cha
kuingizia mapato endapo atapatikana kiongozi mwenye uchungu na
maendeleo ya Yanga na asiwe mpigaji.
“Kwa hiyo, katika uchaguzi ujao ambao utafanyika ili kuziba nafasi
iliyoachwa na Manji, nitagombea nafasi hiyo kwani uwezo wa kuipa Yanga
mafanikio ninao,” alisema Akilimali.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment