Kwa bahati mbaya sana siku inasomwa Ripoti ya 2 sikupata fursa ya
kuisikiliza!! Anyway, labda niseme sikutaka kuisikiliza! Binafsi huwa
nasubiria ripoti kamili ili niisome kituo kwa kituo!!!
Baada ya kuisoma ripoti hiy kituo kwa kituo, nikagundua kwamba, wakati
tunafikiria JK nae ana hatia kwa kusaini hiyo mikataba kama Waziri wa
Nishati na Madini, kumbe Ripoti ya Profesa Osoro ilishamsafisha
kitambo!!!!
Sehemu ya 5 ya Ripoti ya Profesa Osoro (Ripoti ya 2) inazungumzia
Mikataba ya uchimbaji madini (Mining Development Agreements-MDAs).
Kipengele hiki kinaanza kwa kusema:
Mheshimiwa Rais,
Mikataba ya uchimbaji wa madini inafanyika
chini ya kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini, Sura 123. Kwa mikataba
iliyoingiwa mwaka 1994, mikataba hiyo ilifanyika chini ya kifungu cha
kifungu 15 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1979 na kifungu cha 10 cha
Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 .
Hiyo mikataba ya 1994 ndiyo ambayo ilisainiwa na JK!!!
Na kwa maana nyingine, Profesa Osoro na timu yake ni kama wanataka
kutuambia tusimsumbue sumbue JK kwani yeye alisaini kwa kutumia sheria
ya Nyerere isiyo ya kifasadi!!
Nadhani hiyo wakaona haitoshi, wakaamua kumpamba lakini bila kumtaja jina! Hawa hapa tena:
Mgodi wa Bulyanhulu Gold Mines Ltd (Kahama
Mine Corporation Limited). Katika mkataba huu, Waziri wa Nishati na
madini kwa jitihada kubwa alifanikiwa kujadiliana na kampuni hii na
kuiwezesha Serikali kupata asilimia 15 za hisa katika kampuni za
uchimbaji. Hata hivyo, mkataba huoulifanyiwa marekebisho mwezi Juni,
1999 na kusainiwa na Waziri wa Nishati na Madini aliyefuata, Mheshimiwa
Dkt. Abdallah Omari Kigoda.
Hapo Profesa Osoro naona anajaribu kutuambia ni namna gani waziri asiye
na jina jinsi alivyokuwa "ame-figh"t kweli kweli kuhakikisha serikali
inapata 15%!!!
Katika hali ya ajabu kabisa, akaja waziri mwingine ambae ametajwa LIVE
kwamba ni Dr. Abdallah Kigoda! Huyu bila kujali "fight" za waziri asiye
na jina akaamua kuhujumu "struggles" za waziri waliyeshindwa kumtaja!!!
Itoshe tu kusema kwamba, mawaziri wooooooooooooooooote waliopita nishati
including Muhongo wa juzi juzi; hawa wametajwa kwa majina yao kasoro
waziri mmoja tu... aliyesaini mkataba wa Bulyanhulu!!!
Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, ni JK ndie alisaini mkataba wa
Bulyanhulu (am ready to be corrected). Kwahiyo waziri asiye na ajina
ambae ali-struggle kweli kweli ni JK!!!!
Shikamoo JPM!!! Ama kweli hakuna kufukua makaburi hapa!!!!!
Chanzo JF
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment