Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga, leo
Jumatano Juni 14, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 22 watakaounda
kikosi kinachokwenda kushindana kuwania Kombe la Castle Cosafa nchini
Afrika Kusini.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, inatarajiwa kuanza kambi
rasmi kesho Jumapili Juni 18, mwaka huu. Kambi hiyo itakuwa kwenye
Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es
Salaam.
Taifa Stars inajiandaa na michuano ya Cosafa inayotarajiwa kuanza Juni
25, mwaka huu. Michuano hiyo, inaandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la
nchi za Kusini mwa Afrika ambako Tanzania - mwanachama wa Cecafa,
imepata mwaliko kushiriki.
Tanzania imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na
Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe.
Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na
Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali.
Kwa mujibu wa Mayanga, kikosi hicho kinaundwa na makipa Aishi Salum
Manula (Azam FC), Benno David Kakolanya (Young Africans SC) na Said
Mohammed Said (Mtibwa Sugar FC).
Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Salum Kapombe (Azam FC)
na Hassan Hamis Ramadhan ‘Kessy’ (Young Africans SC) wakati upande wa
kushoto wapo Gadiel Michael (Azam FC) na Amim Abdulkarim (Toto Africans
FC).
Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Hassan Abdallah
(Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons)
wakati viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Salmin Hoza wa
Mbao FC.
Kadhalika wako viungo wa kushambulia ambao ni Mzamiru Yassin Selembe
(Simba), Simon Happygod Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya
City) na Shizza Ramadhani Kichuya (Simba SC).
Katika safu ya ushambuliaji wamo Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC
Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Abeid Yusufu (Kagera Sugar), Stamili
Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam FC).
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment