Askari Mgambo, Nurdin Kisinga (33) Mkazi wa Kijiji cha Umwe Kaskazini
Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoani Pwani amelazwa katika Hospital ya
Mchukwi baada ya kupigwa risasi ya kisongoni.
Huyu ni mgambo pili kipigwa risasi ndani ya siku mbili baada ya Erick
Mwarabu kuuawa juzi saa tisa usiku akiwa uvunguni mwa kitanda chake.
Tukio la leo Jumatano limetokea katika eneo la Ngomboloni lililopo
katika Kijiji cha Umwe Kaskazini ikiwa ni takribani saa 19 tangu Mkuu wa
Jeshi la Polisi(IGP), Simon Sirro kufanya mkutano wa mazungumzo na
wazee wa wilaya za Kibiti na Rufiji ili kukomesha mauaji katika wilaya
hizo.
Akielezea jinsi tukio hilo lilivyotokea, kaka wa majeruhi
aliyejitambulisha kwa jina la Kisinga Athumani Kisinga akiwa katika
Hospitali ya Mchukwi alisema ndugu yake alipigwa risasi akiwa shambani
kwake.
Alisema Nurdin alikuwa akivuna ufuta wake shambani kwake ndipo watu
ambao hawajajulikana idadi yao walimpiga risasi moja ya kisogoni na
kutokomea kusikojulikana.
Kisinga alisema Nurdin alikuwa ameambatana na vijana wawili ambao ni watoto wake kuvuna ufuta huo.
Alisema mara baada ya kuanguka chini wadogo zake waliomba msaada kwa
kupiga yowe na ndipo mtu mmoja alifika eneo la tukio na kumchukua kwa
baiskeli hadi barabarani.
Alisema mara baada ya kufika barabarani alifanikiwa kubebwa kwa pikipiki hadi kituo cha Polisi Ikwiriri.
Alifafanua kuwa baada ya hapo alikimbizwa katika kitio cha Afya Ikwiriri
ambapo alipatia huduma ya kwanza kituoni hapo na baadaye alipelekwa
Mchukwi kwa matibabu zaidi.
Mganga wa zamu katika hospitali hiyo Emmanuel Humbi alisema wanampeleka kwenye chumba cha X Ray kwa ajili ya uchunguzi.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment