Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni hiyo, Abbas Tarimba
alisema jana Dar es Salaam kuwa, ni jambo linalosikitisha timu za
Tanzania kutolewa mapema katika michuano hiyo yenye dau kubwa
zikionyesha wazi hazikuwa makini.
Timu za Tanzania zilizoshiriki michuano hiyo ni Yanga, Simba, Singida
United na Jang’ombe Boys zilizoshindwa kutamba kwa timu za Kenya, Gor
Mahia, AFC Leopards, Nakuru All Stars na Tusker. Simba ilitolewa hatua
ya mtoano kwa penalti 5-4 dhidi ya Nakuru All Stars baada ya kutoka
suluhu dakika 90.
Singida United ilitolewa na AFC Leopards kwa penalti 5-4 baada ya sare
ya bao 1-1. Yanga iliwatoaTusker mchezo wa kwanza kwa penalti 4-2 baada
ya kutoka suluhu 0-0 lakini ikatolewa nusu fainali na AFC Leopards kwa
penalti 4-2 zilipotoka 0-0.
Akizungumza uwezekano wa kuzisaidia Simba na Yanga kucheza na Everton,
Tarimba alisema ni mapema mno kulisemea hilo lakini wataangalia cha
kufanya. “Hatukutarajia timu zetu zingetolewa mapema. Kwa kweli
imetushangaza.
Tumeshindwa kucheza kwa kiwango cha juu jambo ambalo limetuhuzunisha.
Inawezekana kabisa hazikufanya matayarisho,” alisema Tarimba. Alisema
wachezaji wenyewe hawakuwa makini kwani ni kama walichezea bahati.
Alisema huenda hazikufanya matayarisho mazuri ingawa zilipewa taarifa
mapema. Alisema hakubaliani na visingizio vya timu hizo kuwa wachezaji
wao walikwenda kujiunga na timu ya Taifa, Taifa Stars kujiandaa na mechi
ya AFCON dhidi ya Lesotho inayoanyika Chamazi, leo usiku.
Alisema hata Gor Mahia ina wachezaji wengi wanaocheza timu ya taifa
Kenya na bado waliopo walicheza kwa kiwango cha juu na kufunga magoli
katika mechi zao. Tarimba alisema ni Singida United tu iliyothubutu
kufunga goli lakini si Simba, Yanga wala Jang’ombe iliyoweza kufanya
hivyo zikionyesha udhaifu katika ufungaji.
Alisema lengo lao ni kusaidia soka la Tanzania na hasa wachezaji kufika
mbali ndio maana walitoa fursa ya michuano hiyo ili wachezaji waitumie
kuonyesha uwezo. Timu zilizotinga fainali ni Gor Mahia na Leopards zote
za Kenya ambazo kesho zitacheza fainali na atakayeibuka bingwa atacheza
na Everton Julai 13, mwaka huu.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment