SIMBA imeamua kufanya kufuru katika usajili wake kwa ajili ya msimu ujao
wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo inasemekana wametumia dau la Dola
50,000 za Marekani (Sh mil 110) kwa ajili ya kumng’oa kiungo
mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima.
Niyonzima ambaye amemaliza mkataba wake na Yanga, yupo nchini kwao
Rwanda alipokwenda kuungana na timu yake ya taifa ‘Amavubi’ kwa ajili ya
mechi ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).
Yanga imeshindwa kuwaongezea mikataba mipya baadhi ya wachezaji wake wa
kimataifa kutokana na kile kinachodaiwa ni ukata ulioikumba klabu hiyo
kwa sasa.
Kufuatia jambo hilo, uongozi wa klabu ya Simba ambao kwa muda mrefu
walikuwa wakihitaji huduma na Mnyarwanda huyo, umefunga safari hadi
nchini kwao kwa ajili ya kumalizana na mchezaji huyo.
Akizungumza kwa njia ya simu kutokea Rwanda, mmoja wa wanafamilia wa
mchezaji huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema tayari viongozi
wa Simba wamemalizana na mchezaji huyo kwa dau la dola 50,000 za
Marekani.
Alisema: “Ni kweli Niyonzima amemalizana na Simba na wamemfuata huku na hivyo kila kitu kimekwenda sawa.”
Kwa upande wake, Niyonzima licha ya kuthibitisha viongozi wa Simba
kumfuata kwao nchini Rwanda, lakini alisema bado hajaingia mkataba rasmi
na timu hiyo.
“Ni kweli viongozi wa Simba wamenifuata Rwanda, nimerudi juzi kutoka
kuitumikia timu yangu ya Taifa, sijasaini mkataba nayo lakini tupo
kwenye mazungumzo,” alisema Niyonzima ambaye ni nahodha wa Amavubi.
Hata hivyo, hivi karibuni mchezaji huyo alihojiwa na gazeti la New Times
Sports la nchini kwao na kuweka wazi mipango yake akisema, ameshawaaga
mashabiki wa Yanga na kwamba muda wake wa kuondoka ndani ya timu hiyo
umefika.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment