Baada ya kuziona nyavu kwa kuifungia Yanga bao, Obey Chirwa amesema anaamini ataendelea kufanya vizuri.
Chirwa
raia wa Zambia amekuwa katika wakati mgumu hadi alipofunga bao wakati
Yanga ikiivaa Mtibwa Sugar na kuitwanga kwa mabao 3-1.
“Najua
tunavyoshirikiana, tunavyofanya kazi yetu kwa pamoja kwa lengo la
kuisaidia timu. Natamani kufunga, pia natamani kutoa pasi za mabao.
Nitasaidiana na wenzangu na kufanya vizuri,” alisema Chirwa.
Mshambuliaji
huyo alifunga bao safi la shuti kali, likiwa la kwanza kwake kwenye
ligi na alikimbia kwenda kumkumbatia kocha wake, Hans van der Pluijm.
Pamoja
na Chirwa kuonekana ni mchezaji mzuri, suala la presha limeonekana
kumpa wakati mgumu na kufunga bao, huenda kukamsaidia kufanya vizuri.
0 comments:
Post a Comment