Nahodha
na kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude, amepongeza maamuzi ya Kamati
ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kutengua adhabu yake
ya kadi nyekundu aliyoipata katika mechi dhidi ya Yanga, Jumamosi
iliyopita.
Mkude
amesema kadi hiyo aliyopewa na Martin Saanya ilikuwa ikimtesa na
kumnyima raha kwa kuwa hakufanya kitendo kilichodaiwa kuwa alikifanya na
kudai kuwa kilichotokea ni kumfedhehesha kwa kiwango cha juu kwa
kumsingizia kosa ambalo hakufanya.
Kadi ya Mkude ilidaiwa kuwa ilitokana na kumsukuma mwamuzi huyo wakati akilalamikia bao lililofungwa na Amissi Tambwe.
“Ile
kadi ilinifedhehesha sana na kuniweka katika wakati mgumu na kunitesa,
nilikuwa nawaza kila siku juu ya mashabiki kuwa wananifikiriaje,
ilionekana nimesababisha timu ikacheza pungufu, nilijua sijafanya kosa
hilo kwa kuwa sikumgusa mwamuzi hata kidogo na ndiyo maana nikawa na
hasira.
“Ifike
hatua pindi itakapofika mechi kubwa kama hizi waletwe waamuzi kutoka
nje ya Tanzania ili kuweza kuchezesha kwa kuondoa utata kama huu kwani
kadi niliyopewa mimi ni wazi nimeonekana kuigharimu timu katika mchezo
ule kwa kucheza pungufu.
“Nilitamani
nipate mkanda wa tukio lile siku ileile baada ya mchezo kwisha
niwaonyeshe Watanzania ili waone juu ya kile kilichotokea, lakini
nimefurahishwa na maamuzi ambayo yananitia faraja sana ambayo yamefanya
ukweli ujulikane na mashabiki wa Simba wafahamu ukweli juu ya hilo,”
alisema Mkude.
SOURCE: CHAMPIONI
0 comments:
Post a Comment