Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>BINTI Karume ‘Amchana’ Lipumba.Fahamu zaidi hapa.
Fatma Karume, mtoto wa rais wa zamani wa Zanzibar, ameshangazwa na
kitendo cha Profesa Ibrahim Lipumba kutaka kurudi kwenye nafasi yake ya
awali ya uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) wakati alijiuzulu
mwenyewe.
Fatma, mtoto wa Amani Abeid Karume ambaye ni rais wa sita wa Zanzibar,
alisema hayo alipoulizwa kuhusu hali iliyoukumba uongozi kwenye chama
hicho kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar baada ya tamko la Msajili wa
Vyama vya Siasa kuwa, anamtambua Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti halali
wa CUF.
Msajili huyo, Jaji Francis Mutungi alitoa uamuzi huo baada ya kuziita
pande zinazosigana kwenye mgogoro, kusikiliza hoja zao baadaye kutoa
maoni na msimamo wa ofisi yake kuwa Profesa Lipumba alifuta uamuzi wake
kwa maandishi kabla ya mkutano mkuu wa CUF haujajadili barua yake ya
kujiuzulu, hivyo anaendelea kuwa mwenyekiti halali.
“Profesa Lipumba alijiuzulu mwenyewe. Aliandika barua akaipeleka kwa
katibu mkuu, kisha akautangazia umma na dunia nzima ikafahamu kwamba
siyo tena mwenyekiti wa CUF,” alisema.
Related Posts:
Polepole Avishukia Vyama vya Upinzani Juu ya Mauaji ya Makada wa CCM na Polisi Yanayoendelea Kibiti.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekemea vikali mauaji yanayotokea mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo, Alhamisi Polepole
amesema kuwa kama CCM wanataka kuona m… Read More
Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo.
Bonyeza Links Zifuatazo
Job Opportunity at CVPeople Africa, Team Leader
Job Opportunity at Knight Support, Zonal Sales Representatives
Job Opportunity at LL COSMETICS, Driver
Job Opportunity at Proactive Employment Sol… Read More
Zitto Kabwe 'Kwa Hili Sisi ni Matajiri Kuliko Afrika Kusini na Ghana'.
"Mwaka 2016, Afrika Kusini ilizalisha tani 140 za dhahabu na Ghana tani
90 hivyo kuongoza Afrika. Kwa Taarifa ya Prof. Mruma, Tanzania huzalisha
tani 112 za dhahabu kutoka kwenye makanikia yaliyokutwa kwenye
… Read More
Hatimaye Boss wa Star TV ajiuzuru kazi baada ya Star kumuhoji RC MAKONDA.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
&nbs… Read More
Lowassa na Lipumba Wakutana Uso kwa Uso Msibani..Lipumba Akimbilia Kumsalimia Harakaharaka.
Baada ya kimya kirefu , hatimaye Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa
amekutana na uso kwa uso na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF)
anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim
Lipumb… Read More
0 comments:
Post a Comment