Thursday 6 October 2016

#YALIYOJIRI>>>>>Bunge Uganda Laimwagia Sifa Tanzania.Fahamu zaidi hapa.

BUNGE la Uganda limeipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na Baraza la Maadili lenye nguvu kuliko nchi nyingine Afrika ambalo linashughulikia watumishi wa umma ikiwemo kupambana na vitendo vya rushwa.
Akizungumza katika mkutano kati ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Uganda na Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma jana Dar es Salaam, Kiongozi wa kamati hiyo, Jacob Oboth-Oboth alisema kuwa katika nchi za Afrika, Tanzania pekee ndio lenye baraza imara na kwamba huenda Nigeria ndio inafuata.

Oboth ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Budama Kusini Wilaya ya Tororo, Uganda, alisema sababu ya kuja nchini ni kujifunza namna sekretarieti hiyo inavyofanya kazi kutokana na kupewa meno na sheria iliyopo kwenye Katiba.

"Uganda tuna mpango wa kufanya marekebisho ya sheria iliyotungwa mwaka 2002 kwa lengo la kuwa na watumishi wawajibikaji na utawala bora na kwamba bila ya kujifunza hawawezi kujua uzoefu uliopo na namna ya kuondokana na changamoto hizo," alisema.

Kamishna wa Maadili ya Utumishi wa Umma nchini, Jaji Salome Kaganda alisema wabunge hao wa Uganda waliomba kuja kubadilishana uzoefu na Sekretarieti ya Maadili ya Tanzania ili kuona inavyofanya kazi.

"Tumewashauri kwamba baraza letu ni chanzo cha Katiba ya mwaka 1977 na makatazo yake yamebainishwa katika katiba. Mfano, mbunge akionekana na hatia kinyume na katiba, anapoteza sifa kwamba haruhusiwi kugombea kwa miaka mitano kupigwa faini au kupewa onyo," alisema Jaji Kaganda.

Alifafanua kuwa walichokuja kujifunza wabunge wa Uganda ni kutokana na sheria yao ya maadili kuwepo kwenye vitabu vya sheria pekee wakati kinachotakiwa, sheria itakayotungwa iendane na katiba yenyewe ili kuipa meno.

0 comments:

Post a Comment