Mgombea
wa ubunge wa jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo
Kalapina akikabidhi sera na ilani ya chama cha ACT Wazalendo kwa
kiongozi wa chama hicho katika soko la Tandale.
Mgombea ubunge jimbo la kawe kupitia chama hicho, Janet Joel Akizungumza
na wakazi wa tandale alipopata nafasi ya kuwasalimia wananchi wa mtaa huo.
Mgombea wa ubunge wa jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo Kalapina akizungumza na wakazi wa tandale wakati wa kufungua Kampeni za chama chicho jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vijana wakimshangilia Kalapina baada ya kumaliza
kuzungumza na kumwaga sera zake kwa wakazi wa tandale.
Na:Elisa Shunda,Dar
MGOMBEA ubunge jimbo la Kinondoni kupitia chama cha
ACT wazalendo, Karama Masudi “Kalapina” azindua kampeni zake katika
eneo soko la Tandale baada ya kushinda kesi ya kuwekewa pingamizi na mgombea ubunge
wa jimbo hilo kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Iddi Azzan.
Akizungumza na wakazi wa eneo hilo mgombea huyo alisema kuwa baada ya kuwekewa
pingamizi lisilokuwa na mantiki yoyote na mgombea mwenzake hatimaye
baada ya kushinda leo wameamua kufungua kampeni zao na watazunguka jimbo zima
kueleza sera za chama chake na mambo muhimu ambayo atayasimamia endapo wananchi wa jimbo
la Kinondoni wakimpa ridhaa ya kuwaongoza.
“Ndugu wananchi baada ya kushinda pingamizi
lililowekwa na mgombea mwenzangu hatimeye nimeshinda, nipende kusema kuwa
mkini kuchagua mbunge wenu nitahakikisha suala la madawa ya kulevya linaisha
katika wilaya yetu kwani matumizi ya madawa ya kulevya yanaondoa nguvu kazi ya
taifa kama nilivyoanzisha kipindi cha televisheni katika kuelimisha vijana
wenzangu kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya ndivyo nitakapoenda
kuwasemea kule bungeni juu ya uingizwaji wa madawa ya kulevya nchini uwe mwisho
ili kuwakomboa vijana wenzangu na dimbwi hili hatari” alisema Masudi.
Aidha mgombea huyo alizitaja sera zake muhimu
atakazosimamia pindi akichaguliwa kuwa mwakilishi wao kuwa ni elimu bora, afya nzuri
kwa wananchi wote na kuhakikisha katika jimbo la Kinondoni linakua na
miundombinu mizuri ya kupitisha majitaka.
“Endapo mkini chagua kuwa mbunge wenu nitahakikisha
nasimamia jimbo letu katika suala la elimu mahitaji yote muhimu kama vitabu, madawati
na kuwepo kwa maabara kwenye shule hizo, upande wa afya nitahakikisha dawa
zinapatikana kwa wingi katika zahanati zetu pamoja na hospitali ya Mwananyamala
na kuhakikisha wakinamama wajawazito hawalali wawili wawili kwenye kitanda
kimoja au kulala chini na mwisho nitahakikisha miundombinu ya jimbo la Kinondoni
inakuwa katika hali nzuri ili kujiepusha na magonjwa nyemelezi kama
kipindupindu nitahakikisha mifereji itakuwa katika hali nzuri na jimbo letu litabadilika
liwe la mfano kama mji wa Manhattan” Alisema Masudi.
Aidha mgombea huyo alimaliza kwa kusema ni wakati
wa mabadiliko kwa wakazi wa jimbo la Kinondoni kumchagua mwakilishi atakayeenda
kuwasemea matatizo yao na siyo kupeleka watu wenye maslahi yao binafsi ambao
wanaenda bungeni kwa ajili ya kuhakikisha biashara zao haramu zinapita kwa
urahisi kutokana na wao kuitwa waheshimiwa, pamoja na mgombea huyo alisindikizwa
kwenye mkutano huo na mgombea ubunge jimbo la Kawe, Janet Joel, mgombea ubunge
jimbo la Tarime,Deo Meck pamoja na kuwaombea kura na kuwanadi wagombea udiwani
kata ya Tandale, Makumbusho na Mwananyamala.
Toa maoni yako hapa.
0 comments:
Post a Comment