Kuna model maarufu wa Bongo aliyetosa kuonekana kwenye video ya wimbo wa Diamond ‘Salome.’
Model huyo anadaiwa kutaka alipwe fedha nyingi ambazo zilikuwa nje ya bajeti ya staa huyo.
“Bajeti yangu haikuweza kumuafford, na siwezi kufanya kitu kimashauzi
wakati bajeti yangu ndogo,” Diamond alikiambia kipindi cha The Playlist
cha Times.
Diamond anasema alichokikosa model huyo baada ya kukataa kufanya video
hiyo si fedha tu, bali exposure ambayo angeipata baada ya hapo.
“Si uchawi, sio uongo, sio ushirikina, unavyofanya video na mimi unakuwa
mkubwa na inakuongezea dau,” alisisitiza kwa kuongeza kuwa watu kibao
humuomba waonekane kwenye video zake bure lakini hukataa kwakuwa ni
lazima awalipe.
Diamond amedai hiyo ndio sababu hatokuja kulitaja jina lake kwakuwa atampa kiki na atakuwa mkubwa.
“Nilimuambia, angalia angle zote mbili, angalia kwamba nakulipa kiasi
lakini kushiriki kwako kwenye hii video itakuongezea ukubwa zaidi,
itakupa biashara nyingi.”
Alitoa mfano kuwa show nyingi za MTV alizowahi kutumbuiza alifanya bure
kwasababu alizitumia kukuza jina lake. Anasema wakati mwingine hadi
dancers huwasafirisha kwa gharama zake mwenyewe.
“Lakini najua show ninayoifanya pale ikitoka itanipa hela nyingi
baadaye. Niliheshimu alichokisema ndio maana sikumind, nilisema
naheshimu sababu umejitambua na umeona thamani yako ni nini, lakini
bahati mbaya sisi bajeti yetu haikufika huko.”
0 comments:
Post a Comment