Katika
kunogesha tamasha la Kandanda Day,wachezaji wanaounda kikosi cha Dar
City FC,wanatarajia kushuka katika dimba la uwanja wa Jakaya M Kikwete
Park,Kidogo Chekundu,Jumamosi wiki hii.
Kiongozi
wa timu hiyo, Athuman Tippo ‘Zizzou’, alisema kwamba wameamua kushiriki
tamasha la mwaka huu ili kuunga mkono,kampeni inayoendelea nchini ya
ukusanyaji fedha kwa ajili ya madawati katika shule mbalimbali nchini.
“Sisi
kama wadau wa soka,tumeamua kushiriki katika tamasha la kandanda
day,ili kutoa mchango wetu kwa jamii kupitia michezo,tunaamini wachezaji
wanaoshiriki tamasha hilo wa Dar City,wanakila sababu ya kuwa sehemu ya
mchango huo,”alisema Tippo na kuongeza:
“Kwa
maana hiyo,kikosi changu ambacho kitashuka dimbani kitakuwa
kimekamilika na kitakuwa kimesheheni wachezaji wengi waliowahi kutamba
na wanaoendelea kutamba katika soka la nchi hii.”
Baadhi
ya wachezaji wanaounda kikosi hicho ambao walipata kuzitumikia klabu za
soka za Simba na Yanga ni Juma Kaseja,Salvatory Edward,Elimboto
Nkumbi,Haruna Moshi’Boban’,George Masatu,Kassa Mussa,Shaaban Kado na
Shaaban Ramadhan.
Tamasha
hilo,linatarajia kushirikisha timu mbalimbali za makampuni na taasisi
lina na kampuni ya matairi nchini Bin Slum Tyres Ltd,kampuni ya simu ya
mikononi Smart,Michuzi Blog,Galacha na Coca Cola.
Imetolewa na Mratibu
Mohamed Mkangara
0 comments:
Post a Comment