Saturday 8 October 2016

#MICHEZO>>>>LIST YA MABEKI 5 BORA DUNIANI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mabeki bora huja kutokana na kuokoa hatari nyingi zitokananzo na washambuliaji ambao wako na njaa ya ajabu ili kuona uzuri wa beki hutokea hapo, sasa mabeki wako wengi nakupa orodha ya mabeki 5 ambao wamefanya vizuri kwa kipindi hiki cha karibuni tangu mwaka huu uanze heshima na busara zao uwanjanani.

5. Laurent Koscielny 

Beki kisiki wa Arsenal amefanya vizuri sana msimu huu hata msimu uliopita ameweza kuokoa hatari nyingi sana kwa sasa ukitaja mabeki 5 lazima utaje jina la beki huyu kwani ameweza kutengeneza kitu haswa ukuta wa Arsenal umekamilika baada ya kuja Shkodran Musatafi. Hivyo Koscienly anabakia kuwa beki bora EPL kwa kipindi hiki kumbuka beki huyu amefunga magoli 34 hadi sasa.

4. Sergio Ramos

Huyu bwana ana balaa sana pale kati anapanda na kuweka kamba kila siku anaweza kufanya chochote akitakacho uwanjani kama beki Ramos anabaki kuwa mhimili mzito sana Real Madrid ameweza kufunga magoli muhimu sana yakiwemo ya UEFA nakumuweka katika nafasi nzuri ya kuzungunzwa vizuri.

3. Leonardo Bonucci

Beki wa Juventus anafanya mazuri pale nachoshangaa kwanini hawi midomoni mwa vilabu vingi kule Ulaya ameweza kutengeneza uhusiano mzuri sana pale Juventus, mchezaji huyu ana makombe 2 ya ligi kuu Italia pamoja na Supercopa 3.

2. Diego Godin

Mtukutu kutoka amerika lakini anachezea pale Atletico Madrid tena kwa mafanikio makubwa nani asiye fahamu kazi yake huyu bwana, anafanya kazi sana pale Vicente Calderon, naye anahesima yake miongoni mwa mabeki bora.

1. Jerome Boateng

Ndio nani asiyejua shughuli ya mtu huyu anacheza kwa hisia kubwa sana na uwezo mkubwa pale Byaern Munich na ameweza kuweka uhusiano mkubwa sana miongoni mwa mabeki kule Bayern anabaki kuwa bora.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE
 

0 comments:

Post a Comment