Kama ilivyo kawaida hawa ndio wafumua nyavu bora EPL haswa baada ya kuona wakishidana ili wapate magoli wakiwa wanatafuta soko la kuweza kusifiwa na kusajiliwa kwa gharama.
Katika wafungaji watano ambao tayari kila mmoja ana goli za kutosha kwa mechi tano ziko tayari Arsenal, Manchester City, Chelsea na United wakionekana katika orodha hizo.
1. Diego Costa
Huyu mtukutu sana lakini msimu huu ametulia na kufanya mambo makubwa
kama aliyokuja nayo msimu wa awali Costa tayari ana magoli 5 yote
akiyapachika kwa jitihada katika orodha hiyo hakuna goli la tuta kwa
maana ya penati.
2. Michail Antonio
Huyu ni mshambuliji wa Westham tayari ameweka kimiani magoli 5 naye kama Costa hakuna goli la penati kwa maana jitihada zake binafsi zimetumika kupata magoli yake.
3. Sergio Aguero
Anafanya vizuri sana akiwepo uwanjani lazima uamini atoke na kitu lakini naye ana magoli 5 kama wenzake lakini sasa ana magoli 3 ya penati katika hayo 5 ambayo amepiga Aguero .
4. Alexis Sanchez
Kwa sasa anacheza kama mshabuliaji wa kati kwa mujibu wa Wenger na kweli humpa matokeo amefunga magoli 4 bila ya penati na inaonekana ataweza kufanya kitu kikubwa sana msimu huu.
5. Zlatan Ibrahimovic
Nyota wa Manchester United amefanya makuu katika historia ya soka tayari ana magoli 4 likiwa moja la penati kiwango chake hakielezeki kama ndio kazaliwa leo .
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment