Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>EDWARD Lowassa Ampongeza Rais John Pombe Magufuli.Fahamu zaidi hapa.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA,
Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kuondoa urasimu katika
taasisi za serikali na kusema hiyo itasaidia kurejesha utendaji kazi kwa
ufanisi.
Lowassa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mtangazaji wa BBC, John
Nene nchi Kenya ambapo alisema urasimu umepungua na hili amejitahiidi
lakini kuna mambo baadhi hayako vizuri.
Lowassa hakuwa tayari kusema ni mambo gani haswa hayakua yakienda sawa
lakini alimkosoa Rais Magufuli kwa kile alichodaiwa kuwa analeta dalili
za udikteta.
Lowassa alikuwa ni mpinzani mkuu wa Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu
mwaka 2015 akigombea kupitia CHADEMA na kuungwa mkono na vyama
vinavyounda UKAWA.
Amekosoa pia uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kupiga marufuku
maandamano, mikutano na vikao vya ndani vya vyama siasa huku vyombo vya
habari vikifungiwa na wale wote wanamkosoa wakifikishwa mahakamani.
Akielezea Opersheni UKUTA, Lowassa alisema kuwa walipanga kuandamana ili
kupinga dalili za udikteta alizoanza kuzionyesha Rais Magufuli.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>>Taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi.Fahamu zaidi hapa.
Mahakama
kuu kanda maalumu ya Iringa leo imesendelea na kesi ya mauaji ya
aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha cha Channel Ten mkoani
Iringa, Daud Mwangosi, inayomkabili askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia
(FFU)… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Askofu Gwajima amjibu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemuita muongo.Fahamu zaidi hapa.
Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemjibu katibu mkuu wa
zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtuhumu kuwa ni mwongo akisema leseni
yake ni ya kuendesha magari makubwa na siyo vibajaji na maguta. … Read More
#YALIYOJIRI>>>Waziri Mkuu kuhamia Dodoma Septemba mwaka huu......Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja.Fahamu zaidi hapa..
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka
huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa
wananchi.
Ametoa
kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) … Read More
Habari Katika Magazeti ya siku ya Leo Jumatatu ya July 25 yako hapa.
… Read More
#YALIYOJIRI>>>Zitto Kabwe na Maalim Seif Kutua Marekani kwa Clinton.Fahamu zaidi hapa.
ZITTO Kabwe na Maalim Seif Sharif Hamad kwa pamoja wameitwa jijini Philadelphia, Marekani.
Maalim Seif ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambapo Zitto ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.
Wanasiasa… Read More
0 comments:
Post a Comment