Monday, 12 September 2016

#YALIYOJIRI>>>>JPM ZIARANI ZAMBIA LEO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Septemba, 2016 anatarajiwa kuwasili Mjini Lusaka nchini Zambia kwa ziara ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia MH. Edgar Chagwa Lungu zitakazofanyika keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji Ia Lusaka.

Rais Magufuli anafanya ziara hii ya kwanza nchini Zambia akiwa mwenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

<<<<DOWNLOAD APPLICTION KWENYE SIMU YAKO HAPA>>>

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment