(Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu serikali kuhamishia akaunti
zote za mapato Benki Kuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya
CRDB, Alex Ngusaru na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa
Wateja, Tully Mwambapa.)
****
SIKU
chache baada ya Serikali kutangaza kuchukua hatua za kupunguza riba za
mabenki kwa wananchi kwa kuagiza akaunti za mashirika na taasisi zake
katika mabenki ya kibiashara zifungwe na kuhamisha fedha zilizopo katika
akaunti hizo kwenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT), benki ya CRDB imeunga
mkono hatua hiyo.
Pia
benki hiyo imewataka wananchi wasiwe na hofu juu ya mpango huo,
kutokana na hofu iliyojengeka kwamba kuna hatari benki za kibiashara
kufilisika nchini.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Dk.Charles Kimei alisema uamuzi uliofanywa na Serikali utasaidia kukuza
uchumi pamoja na kutambua fedha zake mahali zilipo.
Alisema
Serikali ina haki na nia njema kwa kutaka akaunti hizo zifunguliwe BoT
kwa kuwa zimekuwa zikifunguliwa kwenye mabenki makubwa ya kibiashara,
huku baadhi ya Wakala wa ukusanyaji wa fedha wakishindwa kuzifikisha
serikalini kama inavyotakiwa.
Pia
alieleza kuwa mfumo huo hauna utofauti na awali kwani utofauti
utakuwepo kutokana na mashirika na taasisi kufungua akaunti BoT, ambapo
lengo kubwa ni walaka wa Hazina kulenga kuboresha mapato ya serikali
ammbayo yanaweza kutumiwa kwa namna mbalimbali.
“Mfumo
huu…utakuwa hauna tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa fedha zitakazokuwa
zikiingizwa kwenye akaunti hizo ni zile zilizokuwa zikiingizwa kwenye
benki awali, ili kupunguza kiwango cha riba,” alisema.
Pia
alisema hofu nyingine inayojengeka kwa wananchi inatokana na mfumo huo
kutotumiwa kwa muda mrefu na BoT, licha ya kuwa kuna baadhi ya nchi
inatumia mfumo huo na hakuna madhara yoyote.
“Hivyo
tunafikiri maamuzi hayo hayana athari zozote kwani nchi mbalimbali
zimekuwa zikitumia mfumo huo ikiwemo Uganda, Rwanda na Kenya ila kwetu
unaonekana mgeni kutokana na kutotumika kwa muda mrefu,”alisema.
Pia
Dk.Kimei alisema kuwa kutokana na uwepo wa mfumo huo,benki za
kibiashara zitawakopesha zaidi sekta binafsi, ikiwa tofauti na
malalamiko ya mwanzo kwamba Serikali inapata manufaa kutokana na
kukopeshwa zaidi.
“Hii
itasaidia hata wananchi wa kiwango cha chini kuchukua mikopo kutokana
na riba kuwa ndogo, ambapo hata wananchi wa chini wataweza kuchukua
mkopo, ikiwa tofauti na awali wananchi wanashindwa kuchukua mikopo
kutokana na riba kuonekana kuwa juu zaidi ya asilimia 10,”alisema.
Mbali
na hilo, pia Kimei alisema endapo riba ikiwa inapungua itasaidia kukuza
uchumi kutokana na wananchi wengi wa hali ya chini kuchukua mikopo.
0 comments:
Post a Comment