-Ni unaofanywa bila vibali na mfanyabiashara anayedaiwa kuziba njia, kumnyanyasa bibi mjane
-Aagiza OCD amkamate kwa tuhuma za kudai serikali iko mfukoni mwake.
Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapileo asubuhi amewatembelea wananchi wa Tegeta kwa ndevu eneo ambalo bibi anayefahamika kwa jina la Habiba Mustafa alionekana kwenye taarifa ya habari ya itv jana kulalamika kufanyiwa hila njama na mfanyabiashara mmoja ajulikanae kwa jina la Emily Reshea aliyechimba shimo mbele ya nyumba yake na kuziba njia za wananchi kupita kama mbinu ya kuwalazimisha wamuuzie maeneo yao.
Hapi akiwa katika eneo hilo akiambatana na wataalamu wa mipango miji, muhandisi wa manispaa na askari wa jeshi la polisi ameagiza kuvunjwa kwa ukuta ulioziba njia za wananchi kupita, kufukiwa kwa shimo lililochimbwa kabla ya saa 12 jioni leo na kumtaka OCD Kawe kuchunguza tuhuma za mfanyabiashara huyo kudaiwa kusema kuwa
"serikali iko mfukoni mwake"
na ikibainika kuwa ni kweli akamatwe mara moja na kuhojiwa na vyombo vya dola.
Wataalamu wa makazi na mazingira wa manispaa ya Kinondoni wamesema mfanyabiashara huyo atazuiwa kuendelea na ujenzi na wamemtaka kuwasiliha nyaraka zake zote katika ofisi za manispaa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni amefika Tegeta baada ya kusikia kilio cha mama huyo mjane kwenye kituo cha Televisheni ya ITV jana usiku.
Bibi Habiba amemshukuru Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa kusikia kilio chake na kufika kumsaidia.
0 comments:
Post a Comment