Wakala
wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetoa muda wa miezi miwili
kwa wafanyabiashara wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajiliwa
wafanye hivyo haraka.
Akizungumza
na waandishi wa waandishi wa jijini Dar es salaam jana, Ofisa Mtendaji
Mkuu wa BRELA, Bw. Frank Kanyusi alisema katika zoezi la kutoa elimu na
kurasimisha majina ya biashara na kampuni linaloendelea katika mikoa
mbalimbali imebainika kuwa wafanyabiashara wengi wanatumia majina ya
biashara pasipo kuyasajili.
“Sheria ya majina ya biashara inamtaka mfanyabiashara kusajili jina la biashara yake ndani ya siku 28 toka aanze kulitumia,” alisema Bw.Kanyusi na kuongezea kuwa kinyume na hapo atakuwa amevunja sheria ya majina ya biashara.
Alisema
baada ya muda huo kupita, patakuwa na msako nchi nzima ili kuwabaini
wale wote wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajili na kuwafikisha
katika vyombo vya sheria au kuwatoza faini.
Alisema
kuwa sasa usajili wa majina ya biashara umerahisishwa kwani unafanywa
kwa njia ya mtandao kwa kutembelea tovuti ya wakala huo ambayo ni www.brela.go.tz ili kupata maelezo yote ya namna ya kusajili jina la biashara.
Aliwataka
wafanyabiashara wasiishie kusajili tu jina la biashara bali pia waende
katika Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa ajili ya kupata namba ya Mlipa Kodi
(TIN) pia waendele katika halmashauri zao kupata leseni ya biashara.
“Kwa
kurasimisha biashara serikali itapata mapato kwani wigo wa walipa kodi
utaongezeka na pia itakuwa faida kwa wafanyabiashara katika kujengewa
mazingira bora ya kufanya biashara,” alisisitiza Bw.Kanyusi.
Alisema
BRELA imejipanga kuzunguka mikoa yote nchini ili kutoa elimu juu ya
urasimishaji wa majina ya biashara na makampuni kwani imeonekana
wananchi hawana uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa urasimishaji.
Hadi
sasa BRELA imefanya ziara katika mikoa ya Mwanza, Mara, Geita na Simiyu
na wiki hii watakuwa mkoani Shinyanga kwa muda wiki moja katika
kuhamasisha wafanyabiashara kurasimisha biashara zao.
Alisisitiza
kuwa ni lazima kuhakikisha kuwa biashara zinarasimishwa ili serikali
iweze kuwatambua walipa kodi wake ambao watachangia pato la taifa na
kuiwezesha Tanzania kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
0 comments:
Post a Comment