Rais
Dk. John Magufuli, amemteua aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kumwakilisha katika mkutano
wa makazi wa Habitat III unaofanyika katika mji wa Quito, Ecuador.
Taarifa
iliyoituma kwenye mitandao ya jamii na Profesa Tibaijuka jana, ilisema
katika msafara huo amefuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Mandeleo ya Makazi, Dk. Yamungu Kayandabila.
“Hivi
sasa niko Geneva, Uswisi kwa matayarisho nikielekea Quito Ecuador
mkutano wa makazi duniani wa HABITAT III kumwakilisha Rais wetu nikiwa
pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,namshukuru Rais kwa heshima hii
kubwa, Sitamuangusha.
Habitat III,ni mkutano wa uamuzi na mustakabali wa Shirika la Makazi Duniani na agenda ya maendeleo endelevu ya miji.
“Kama
tunavyojua mkutano wa Habita I ulifanyika Vancouver,Canada mwaka 1976,
Habitat II ulifanyika Istanbul, Uturuki mwaka 1996 na huu Ecuador
Marekani ya Kusini 2016,”alisema.
Alisema
kila baada ya miaka 20 wakuu wa nchi hukutana kukubaliana namna ya
kuendeleza makazi kupitia Shirika la UNHABITAT ambalo aliwahi kuliongoza
kwa miaka 10.
“Rais
Magufuli alichaguliwa na kuongoza Baraza la Uongozi wa shirika hilo
(Governing Council) kwa muhula wa mwaka 2006/2008 alipokuwa Waziri wa
Ardhi.
“Wafanyakazi
walimpenda kiasi kwamba alipobadilishwa wizara na kupelekwa Mifugo na
Uvuvi karibu iwe zogo ofisini kwangu wakidai tutayumba.
“Niliwatuliza na kuwaambia kumbadilisha wizara hakumuondolei uenyekiti wake na kweli aliendelea nao na kumaliza,”alisema Tibaijuka.
Alisema
katika mkutano huo, jambo kubwa atakalolipigania ni utaratibu wa
shirika hilo kuzisaidia nchi zinazoendelea kama sisi kwa kuzikopesha
halmashauri zao fedha za miundombinu, bila kuilazimisha Serikali kuu
kutoa dhamana kwa mikopo hiyo.
Alisema
jambo hilo ni la msingi kwa vile huleta kasi ya maendeleo ingawa
huwa linapingwa na wakubwa wanaotaka kukopa kupitia Serikali kuu ili
waibane kwa kutumia Benki ya Dunia, kitendo ambacho kinachelewesha
kasi ya maendeleo.
“Tutajitahidi
kulingana na maelekezo ya Rais tunayemwakilisha kuhusu msimamo wa nchi
yetu na washirika wake ambao ni nchi za Afrika na za G77 na China,” alisema.
0 comments:
Post a Comment