Umoja
wa Vijana wa CUF (JuviCUF) umewataka vijana wa chama hicho kutotoa
ushirikiano kwenye ziara ya mwenyekiti aliyevuliwa uongozi na Barza Kuu,
Profesa Ibrahim Lipumba na baadhi ya wabunge inayotarajiwa kuanza wiki
hii mikoa ya Lindi, Mtwara na Tanga.
Wito
huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Juvi-CUF, Hamidu Bobali alipokuwa
anazungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa ziara hiyo ina lengo
la kukipasua chama hiko rasmi.
“Tunajua ziara hiyo inataka kuongeza mpasuko ndani ya chama na mpasuko huo utawapa mwanya maadui zetu ‘kutupiku’ kisiasa,” alisema Bobali.
Bobali,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mchinga kwa tiketi ya chama hicho,
alisema pamoja na harakati za Lipumba tayari wabunge wa mikoa hiyo wapo
katika kikao kuandaa mikakati ya kuimarisha chama.
Kadhalika
Bobali alifafanua kuwa kama Jumuiya wanalaani kitendo kilichofanywa na
kikundi cha vijana kilichojiita cha Mkoa wa Dar es Salaam cha kutoa
kashfa kwa viongozi wa Ukawa akiwamo Freeman Mbowe na Julius Mtatiro.
Juvi-CUF
iliwatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuhusu hali ya kisiasa iliyopo
visiwani humo, kutokana na hatua mbalimbali za kisheria zinazofuatwa ili
kuhakikisha haki inapatikana kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Kuhusu
sakata la akaunti ya chama inayoingizwa fedha za ruzuku na za wabunge,
alisema hakuna fedha za wabunge zitakazoingia katika akaunti hiyo
kutokana na mikataba inayosainiwa inahusu Mbunge na Ofisi ya Bunge na
siyo chama.
“Tumechukua
hatua kuwaeleza benki kuhusu akaunti kufunguliwa, suala hili linafanywa
na bodi ya wadhamini inayoongozwa na Khatau hivyo siyo suala rahisi
yeye (Lipumba) akazipata,” alisema Khatau.
0 comments:
Post a Comment