Chama
cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeitisha mkutano wa dharula wa
wanasheria nchi nzima kwa ajili ya kujadili mapendekezo na kutoa msimamo
wao dhidi ya Serikali ya kuanzisha Bodi ya Usajili ya Mawakili.
Akizumza
jana kwenye mkutano huo Rais wa TLS, Tundu Lissu alisema mapendekezo
yaliyotolewa ni hatari kwa uhuru wa TLS na kada ya sheria kwa ujumla
iwapo siasa itaingia kwenye kazi zao za sheria.
Alisema
bodi hiyo ikianzishwa itakuwa chini ya waziri wa sheria na katiba na
ndiyo itakuwa na nguvu ya kusajili au kuwafuta wanasheria kadri
itakavyoona inafaa.
"Mabadiliko
haya ni hatari sana kwa uhuru wa wanasheria nchini, tumekutana hapa
kuelezana na kupokea maoni ya wanachama kisha tutaweka msimamo wetu
baada ya baraza la TLS kukaa .
"Huo
ni mkakati wa Serikali kuminya uhuru wa TLS ili kuwadhibiti wanasheria
kuingia kwenye siasa, jambo ambalo linatakiwa kupingwa na kila mtu kwa
sababu matokeo yake ni mabaya" alisema Mh. Tundu Lissu.
Mbali
na hayo Lissu aliwaasa wanasheria kuwa endapo watashindwa kusimamia
taaluma yao vizuri na kuruhusu siasa ikaingia ndani yake basi haitokuwa
na maana ya kuwepo kwa chama hicho.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment