Baada ya ukimya, Azam FC imeanza rasmi usajili kuimarisha kikosi chake.
Klabu hiyo ya Mbande, imemnasa mshambuliaji anayekuja kwa kasi hivi sasa nchini, Wazir Junior.
Junior
aliyependekezwa na Kocha Mkuu Aristica Cioaba, anakuwa mchezaji wa
kwanza kusajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao 2017-18, ambapo
alikuwa straika kinara wa Toto African ya Mwanza msimu uliopita, akiwa
mfungaji wao bora kwa mabao sita aliyofunga.
Zoezi
la kuingia mkataba kwa pande hizo mbili limefanyika leo mchana kwenye
Ofisi za Mzizima, zilizopo barabara ya Nyerere, Dar es Salaam, na
kusimamiwa na Meneja Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohamed, aliyekuwa sambamba
na viongozi wengine Meneja wa timu, Phillip Alando na Ofisa Habari,
Jaffar Idd.
Azam
FC ambayo imeanzisha falsafa ya kutengeneza timu ya muda mrefu yenye
wachezaji vijana wenye vipaji pamoja na kuwekeza ipasavyo kwenye kituo
chake cha kukuza vipaji ‘Azam Academy’ kwa kupandisha wachezaji bora,
inaamini ya kuwa ujio wa mshambuliaji huyo utaongeza zaidi makali kwenye
eneo la ushambuliaji.
Mshambuliaji
huyo anaungana na washambuliaji wengine kikosini, Yahaya Mohammed,
Shaaban Idd, Samuel Afful na Yahaya Zaidi, aliyepandishwa kwenye timu
kubwa kwa ajili ya msimu ujao akitokea katika kituo cha kukuza vipaji
vya ‘Azam Academy’.
Wachezaji
wengine ambao tayari wameongezwa kwenye timu kubwa kuelekea msimu ujao
wakitokea kituo hicho, ni mabeki Abbas Kapombe, Abdul Haji, Godfrey
Elias, kiraka Ramadhan Mohamed na kiungo Stanslaus Ladislaus.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment