Chama cha NCCR mageuzi kimezindua kampeni zake katika jimbo la vunjo
mkoani Kilimanjaro na kuwataka watanzania kuchagua viongozi wenye sifa
watakaoweza kusimamia raslimali zilizopo hapa nchini ili ziwanufaishe
wananchi kuondokana na umaskini na kuepusha taifa kutegemea fedha za
wahisani kusaidia bajeti ya nchi.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR mageuzi ambaye pia ni mgombea ubunge
wa jimbo la Vunjo Mh.James Mbatia amesema Tanzania ni nchi tajiri sana
ambayo ina uwezeo wa kujiendesha yenyewe bila kutegemea fedha za
wahisani endapo raslimali zilziopo hapa nchini zitasimamiwa vizuri.
Amesema amefanya utafiti na kubaini fedha ambazo zimetumiwa na
viongozi katika safari za kwenda nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 10
zimegharimu zaidi ya shilingi trilioni 10 na kwamba endapo fedha hizo
zingetumika vizuri zingeweza kujenga hospitali za rufaa katika wilaya
zote hapa nchini.
Amesema endapo watanzania watampa mgomea urais wa vyama vinavyunda
umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Mh.Edward Lowassa ridhaa ya kuiongoza
Tanzania watahakikisha wanaleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu
ikiwa ni pamoja na kulipa madeni yote ya walimu na kuondoa kodi
inayokatwa kwenye mishahara ya wafanyazi.
Kwa upande wake mbunge wa bunge la jumuiya ya Afrika Bashariki Bi
Nderakindo Kessy amesema umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ndiyo njia
pekee ya kuleta demokrasia ya kweli hapa nchini na kuondoa mipaka
iliyowekwa na wakoloni katika nchi za Afrika.
Mjumbe wa halimashauri kuu ya chama cha NCCR mageuzi taifa Hemed
Msabaha na mkurugenzi wa uchumi na fedha kutoka chama cha demokrasia na
maendeleo Chadema Bw.Antony Komu wamesema miaka 50 ya uhuru bado taifa
linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mzigo mkubwa wa deni la
zaidi ya shilingi tlirilioni 35.
Chanzo
ITV HABARI
0 comments:
Post a Comment