Wednesday, 30 March 2016

BREAKING NEWS>>>Gerald Hando, Paul James waacha kazi Clouds FM.Fahamu zaidi hapa.

Watangazaji hao, Gerald Hando na Paul James, maarufu kwa jina la PJ, hawakushiriki kwenye kipindi cha jana asubuhi na Mwananchi ilithibitishiwa baadaye kuwa wamemaliza mikataba yao na uongozi wa kituo hicho hauna mpango wa kuwabakiza.

Dar es Salaam. Watangazaji wawili wa kipindi maarufu cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds FM wameachana na redio hiyo, Mwananchi imetaarifiwa.

Watangazaji hao, Gerald Hando na Paul James, maarufu kwa jina la PJ, hawakushiriki kwenye kipindi cha jana asubuhi na Mwananchi ilithibitishiwa baadaye kuwa wamemaliza mikataba yao na uongozi wa kituo hicho hauna mpango wa kuwabakiza.


Awali, habari zilienea kuwa wawili hao wamefukuzwa kazi kutokana na matatizo ya kinidhamu. Lakini alipoulizwa kuhusu suala hilo, Hando alijibu: “Sijafukuzwa kazi hata kidogo, wala sijaacha kazi. Ninachofahamu mimi ni mfanyakazi wa Clouds Redio na leo (jana) sikusikika kwenye kipindi kwa sababu nilikuwa na udhuru.”


Uongozi wa Clouds unatarajia kutoa taarifa rasmi leo asubuhi kwenye kipindi cha Power Breakfast.


Train la abilia lasimama kituo cha Barkhresa kwa muda wa saa moja kupisha Train linalotoka Kigoma.Fahamu zaidi hapa.

 Train la abilia linalofanya  safari zake kutoka Station mpaka Ubungo Maziwa lasimama saa moja nanusu kupisha train linalotoka  Kigoma huku baadhi ya abilia wakilalamika kukaa muda mrefu kituo cha Buguruni Barkhresa huku abilia wakiambiwa wasubili Train linalotoka Kigoma lipite muda wa jioni. 

Download ngoma ya Navy Kenzo inayoitwa "Kamatia".Hapa hapa.


Zifahamu nchi 10 za Afrika zenye wanawake warembo, Tanzania ikiwemo.Fahamu zaidi hapa.

 Afrika ni bara zuri ambalo limejaa tamaduni mbali mbali, Lugha na watu wa kila aina. Kama ilivyo kila kitu kinakuzidiana, Hivyo katika nchi zilizomo ndani ya bara la Afrika kuna nchi ambazo zinaongoza kuwa na wanawake wenye mvuto. Tunavyo ongelea 'Wazuri/Warembo' hapa ndipo mchanganyano unapo tokea maana ni neno kubwa sana na zito.

Kila moja huona uzuri kwa tofauti yake, Lakini kwa ujumla hatuangalii sura, umbo bali tabia, kujitunza na ushawishi wa kutumia muonekano wako.

NOTE: Mtazamo huu wa Top 10 nchi za Afrika zenye warembo ni kutokana na maoni mengi kutoka kwa watu kwa mujibu wa Afrojuju.net, Hivyo na wewe unaweza kuaj na Top 10 yako yenye nchi ambayo unahizi inawarembo wakali hapa Afrika.

 10: TANZANIA.
Wanawake wa nchi hii wanasifika kwa uzuri, kutunza nyumba na ujuzi kwenye kitanda. Kama unatafuta mwanamke wa kumpeleka nyumbani kumtambulisha ambaye anajua kutunza nyumba, Basi Tanzania ndipo eneo sahihi.

 09: KENYA.
Wasichana wa Kenya niwazuri na wanamahaba, Kama unatafuta msichana ambaye ni mzuri, mwenye mahaba, na anaye jisimamia 'Independent', Mchapa kazi na sio mvivu... Basi kimbilia nchini Kenya.

 08: GHANA.
Haitawezekana kukamilisha list ya nchi zenye warembo bila kupitia Gold Cost. Wanasifa ya kuwa Warefu, Wataalamu kitandani, ngozi ya asilia 'Ebony Skin tone' na wana uhalisi wa Muafrika.




08: GHANA.
Haitawezekana kukamilisha list ya nchi zenye warembo bila kupitia Gold Cost. Wanasifa ya kuwa Warefu, Wataalamu kitandani, ngozi ya asilia 'Ebony Skin tone' na wana uhalisi wa Muafrika.



06: SOUTH AFRICA 'The famous Rainbow Nation'.
Afrika Mashariki ni nyumbani kwa wanawake warembo barani Afrika, kuwanzia Cape Town, Johannesburg, Pretoria na Durban. Wanawake wa Afrika Mashariki utawapata wenye uweupe wa chotara au uweusi halisi wa Afrika.
 04: CAPE VERDE ISLAND.
Sio nchi maarufu barani Afrika wala hata kupata wataa kwenda kuitazama, Lakini kisiwa hicho kidogo ni nyumba ya wasichana na wanawake warembo walioumbwa Afrika. Wanakauli nzuri ya ukarimu ambayo itakufanya usahau njaa wakati hukula chakula.

 03: ETHIOPIA 'The cradle of humanity'.
Ustaarabu ndipo ulipo anzia nchini Ethiopia, Wasichana wa nchi hii sio wazuri tu kwa bara la Afrika bali hata ulimwenguni wamekuwa wakisifika kwa uzuri wao unao shawishi kutangaza ndoa. Wengine wamekuwa wakidai uzuri wao umetokana na mchanganyiko wa mbegu 'uzazi' kutoka kwa watu wa Yeamen na Ethiopia wenyewe.

 02: SOMALIA 'Vita haiondoi urembo'.
Kama hujawahi kukutana na msichana wa Kisomali basi utakapo kutana naye utachanganyikiwa na kukusababisha uweze hata kusaliti uliye naye. Chukulia mfano wa Iman, Model aliye tikisa ulimwengu kwa mwendo wake wa madaha hadi kila mmoja kushangaa. Wanasifika kuwa na macho mazuri, ngozi ya chocolate, nywele laini na ndefu.

01: RWANDA 'Africa's hidden Apple'.
Niwazuri na wakuvutia, Weusi wa asili, Wana umbo nzuri na ukarimu, Sauti ya kimahaba na urefu wakupagawisha. Wakitembea ni sawa na Twiga nyikani akiwa anatembea. Uzuri wao huwezi kuuelezea.

-Nimekosea? Wewe unadhani nchi gani Afrika ingekuwepo kwenye Top 10 yangu ya leo? Niachie comment hapo chini.

#YALIYOJIRI>>> Tanzania yapokea msaada wa shilingi bilioni 116.4 kutoka Japan.Fahamu zaidi hapa.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano na Serikali ya Japan itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara, kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa ajira nchini.

Mkataba wa pili  unahusu masuala ya kiufundi  yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya mkataba uliosainiwa  Octoba 20, 1966, kwa kuzingatia sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Aidha, makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa nchini Tanzania.

Katibu Mkuu Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo Watanzania.

Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.

Balozi Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji  kuwekeza nchini Tanzania.

Adha Balozi Yoshida amesema kuwa Japan itaendelea kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akikisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.

#YALIYOJIRI>>>Diwani wa CHADEMA Apeta Mahakamani, wa CCM Chali baada ya Pingamizi Lake Kutupwa.Fahamu zaidi hapa.

Mahakama  ya Hakimu Mkazi Arusha imetupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya udiwani katika kata ya Musa wilayani Arumeru Magharibi iliyofunguliwa na mgombea wa CCM, Flora Zelote dhidi ya diwani wa Chadema, Loth Laizer.

Akitoa uamuzi wa hukumu hiyo iliyosomwa jana na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Mwamkuga Gunta, alisema haoni kama kuna kasoro yoyote katika uchaguzi huo uliompa ushindi Laizer.

Akitoa uamuzi, Gunta alisema licha ya Zelote kudai kudhalilishwa pamoja na kuibiwa kura lakini ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi mbalimbali hautoshi kudai kuwa alipokwa ushindi wa kuwa diwani wa kata hiyo.

“Natupilia mbali kesi hii sababu ushahidi uliotolewa mahakamani hapa hautoshi kumvua udiwani diwani wa Chadema, pia mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani hapa ushahidi wao umejichanganya hivyo natupilia mbali kesi hii,” alisema Gunta.

Awali kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo wiki iliyopita, Hakimu Gunta aliomba radhi kwa kutokamilisha hukumu hiyo kwa sababu alikuwa akiuguliwa hivyo aliahidi kutoa hukumu jana, Machi 29.

Kesi hiyo ambayo awali ilisikilizwa kwa siku mbili mfululizo kwa zaidi ya saa nane kila siku, mashahidi wote walikamilisha ushahidi wao akiwamo Laizer aliyekiri mahakamani hapo kuwa aliongozana na kundi kubwa la wafuasi wa chama chake kwenda katika kituo kikuu cha kujumlishia matokeo ya udiwani katika kata hiyo kilichokuwa katika shule ya sekondari ya Musa.

Hata hivyo, akiongozwa na wakili wake Adiel Charles, diwani huyo alishindwa kukanusha lugha ya matusi iliyotolewa na wafuasi wake aliyokuwa ameongozana nao Oktoba 25 mwaka jana, wakiwa na silaha za jadi ambazo ni sime na fimbo pamoja na kutishia usalama wa maisha ya mgombea wa CCM, Zelote.

Wengine waliotoa ushahidi wa upande wa mlalamikiwa ni pamoja na msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Musa, Tuwati Leondoya. 

Wengine ni Lomito Robert na Ally Mollel. Kwa upande wa mlalamikaji, mashahidi watano walitoa ushahidi akiwamo Zelote, Meimoite Kivuyo, Lekisongo Singa, Edson Lesikari na Alex Lukumay.

Kesi hiyo ya uchaguzi namba sita ya mwaka 2015 ilifunguliwa mahakamani hapo na Zelote aliyekuwa mgombea wa udiwani katika kata hiyo kwa tiketi ya CCM dhidi ya Laizer wa Chadema.

Zelote alifungua kesi hiyo baada ya kubaini kuwapo kwa ukiukwaji mkubwa wa taratibu za kampeni pamoja na uchaguzi zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Laizer alitangazwa mshindi katika uchaguzi huo.

#YALIYOJIRI>>>Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa afanya ziara ya kushtukiza KOJ Kurasini.Fahamu zaidi hapa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amemuagiza Kaimu Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Nelson Mlali kufanya uhakiki wa kampuni zinazotoa huduma mbalimbali bandarini ili kuboresha utendaji kazi na kuepuka mgongano wa maslahi binafsi minongoni wa watumishi wa bandari.

Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana jioni(29/03/2016) kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini.

“Mtafanyaje kazi na mtu ambaye ni mfanyakazi na huku kampuni yake inatoa huduma bandarini, hamuoni kutakuwa na mgongano wa kimaslahi binafsi,” alihoji Profesa Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa amemtaka Kaimu Meneja Msaidizi Mlali azingatie umiliki wa makampuni kulingana na taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Kampuni nchini (BRELA) katika zoezi la kuhakiki kampuni hizo.

Akiwa eneo la (KOJ) Kurasini, Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa TPA  wabadilike na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa badala ya kufanya kazi kwa mazoea ili kuboresha kuongeza ufanisi na kuliongezea taifa mapato kwa manufaa ya wananchi.

Prof. Mbarawa amewaagiza pia Mamlaka ya Bandari wanaponunua vipuri na vifaa mbalimbali vinavyohitajika bandarini hapo wazingatie vipimo sahihi kulingana na vifaa vinavyohitajika kuendeshea mitambo mbalimbali ili kulipunguzia taifa gharama zisizohitajika.

Mamlaka ya Bandari nchini ina bandari mbalimbali zilizopo katika ukanda wa bahari ya Hindi na maziwa yaliyopo nchini.

Ukanda wa Bahari ya Hindi una bandari ya kuu za Dar es salaam, Tanga na Mtwara pamoja na Bandari ndogo zilizopo Lindi, Kilwa Masoko, Mafia, Bagamoyo, Pangani na Kwale.

Bandari nyingine ziliozo katika maziwa mbalimbali nchini ni pamoja na Ziwa Victoria lenye bandari ya Mwanza, Bukoba, Kemondo, Musoma na Nansio, Ziwa Tanganyika likihusisha bandari ya Kigoma na Kasanga wakati Ziwa Nyasa kuna bandari ya  Itungi, Manda, Liuli na Mbaba Bay.

Mwimbaji Rose Mhando Ashtakiwa Kwa Waziri Nape Juu ya Utapeli Anaofanya.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa nyimbo za injili nchini, Rose Mhando, ameshtakiwa kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, kwa kitendo cha utapeli na kushindwa kutekeleza mkataba wa kuhudhuria na kutumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika jijini Mwanza licha ya kulipwa gharama zote alizotaka.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayoongozwa na Alex Msama, ambayo ina mkataba naye imekuwa ikiuza na kuandaa matamasha ya msanii huyo pamoja na tamasha la Pasaka la kila mwaka, alimweleza Waziri Nnauye, mbele ya halaiki ya wananchi alipokuwa mgeni rasmi wa sherehe za tamasha hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza jijini Mwanza na mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Msama alieleza kusikitishwa na kitendo cha Rose Mhando kuingia mitini ilihali akiwa ameingia mkataba na kulipwa gharama zote pamoja na nauli alizodai kabla ya kuanza safari kufika Geita, Mwanza na Kahama kujiunga na wasanii wenzake kwa ajili ya kutumbuiza katika tamasha hilo.

“Mheshimiwa Waziri, Rose Mhando naye amekuwa ni jipu kwa kuwa amefanya utapeli kwa kukubali kulipwa gharama zake zote lakini ameshindwa kuhudhuria na kutumbuiza kama wenzake wakina Solomon Mkubwa, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone na wengine uliowashuhudia hapa.

“Hii ni mara ya tatu amekuwa akifanya hivi na mara kwa mara nimekuwa nikimsamehe,” alisema bila kutaja kiasi alichomlipa katika mkataba waliokubaliana ili aweze kufanya onyesho hilo.

Msama pia akatumia fursa hiyo kuwaomba radhi wananchi waliofika katika Uwanja wa CCM Kirumba kwa kutegemea mwimbaji huyo angekuwepo na kutumbuiza na wenzake lakini kilichotokea ni aibu na utapeli wa msanii huyo mkubwa wa nyimbo za injili aliyejizolea umaarufu ndani na nje ya nchi.

“Kuanzia leo mtu yeyote asije akaingizwa mjini na Rose Mhando kwa kuingia naye makubaliano akidhani yupo chini ya Kampuni ya Msama Promotions, kwa kitendo alichoendelea kukifanya naomba kutangaza rasmi kuvunja mkataba wa kufanya kazi na msanii huyo ili kulinda hadhi na heshima ya Kampuni yangu,” alisisitiza Msama.

Msama aliomba wananchi waendelee kuipa sapoti kampuni yake kwa kuwa imekuwa ikirejesha mapato ya viingilio na sadaka katika tamasha hilo kwa jamii hasa kwa watu wasiojiweza, makundi maalumu pamoja na kuendeleza vipaji vya wasanii chipukizi wa nyimbo za injili nchini kote.

Hata hivyo, wadau mbalimbali waliokuwepo katika uzinduzi huo walisikitishwa na kutokutokea kwa mwanamuziki huyo huku wengine wakimlalamikia kuwa na tabia hizo kwa muda mrefu na kufanya bila woga na hofu yoyote.

Mwanamuziki huyo aliwahi kuripotiwa kutuhumiwa kufanya udanganyifu kwa kupokea zaidi ya Sh milioni 3 na kisha kushindwa kufanya onyesho katika tamasha la nyimbo za injili lililoandaliwa mkoani Njombe mwaka jana.

Mkurugenzi wa Kampuni ya The Comfort Gospel Promotions, Seth Sedekia, ndiye alimfungulia kesi hiyo  katika kituo kikuu cha polisi Njombe na akapewa RB namba: NJ/RB/1793/2015.

Kushindwa kutokea kwa mwanamuziki huyo siku hiyo ya Jumapili iliyopita, kuliwafanya mashabiki waliokuwa wamelipa kiingilio cha shilingi 5,000 kila mmoja kuzusha vurugu kubwa kwa mwandaaji huyo wakidai wametapeliwa huku wengine wakionyesha kuchukizwa na kitendo cha mwanamuziki huyo kushindwa kutokea kufanya onyesho hilo.

Mwandaaji wa onyesho hilo, Sedekia alisema amefikia hatua ya kufungua kesi kituo cha polisi kufuatia kumlipa fedha zote shilingi milioni tatu Mhando ambazo alisaini mkataba naye akiwa mjini Dodoma kwa ajili ya kufanya onyesho mjini Njombe. Katika onyesho hilo, Mhando alitarajiwa kushirikiana na msanii wa nyimbo za injili, Happy Kamili kutoka jijini Mbeya ambaye alifika katika tamasha hilo akishirikiana na wasanii wengine kutoka mjini Njombe.

Ofisa Habari wa Kamanda wa Polisi mkoani Njombe, Franco Malimba, alipoulizwa juu ya kuwepo kwa taarifa hizo katika kituo cha polisi, alikiri kuwepo lakini alisema hawezi kulizungumzia kwa sababu halijafika ngazi za juu.

#YALIYOJIRI>>>>Waliompiga Daktari Mkoani Mtwara Wakamatwa Wakijiandaa Kutoroka Kwenda Nje ya Nchi.Fahamu zaidi hapa.

Kufuatia tukio la ndugu wa mgonjwa  kumpiga Daktari Mkoani Mtwara, tayari jeshi la Polisi Mkoani humo linawashikilia watu kadhaa kwa kitendo hicho cha kumpiga Daktari wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara,Henry Mwaibambe (Pichani) amesema hadi sasa watu 2 wanaotuhumiwa kumpiga daktari hospitali ya Mkoa wamekamatwa usiku wa kuamkia jana wakitoroka nchini huku wengine 3 wakiendelea kusakwa.

Awali wauguzi na Madaktari wa Hospitali hiyo waligoma kufanya kazi hadi hapo watakapohakikishiwa usalama wao ndipo wafanye kazi

Jana, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliweza kufika Hospitalini hapo na kusuluhisha mgogoro huo huku akiomba Jeshi la Polisi kuongeza usalama kwa watumishi hao wa Afya.

#MICHEZO>>>HATIMAYE NIGERIA WATOLEWA NA MISRI KWA KUPIGWA GOLI 1 BILA ..ZAMU YA TANZANIA KUJITAHIDI SASA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kwa Matokeo ya leo Nigeria wametolewa kwenye Mchakato wa Mashindano ya AFCON 2017. Nafikiri wakatusaidia Lagos.

#YALIYOJIRI>>> Waziri wa Mambo ya nje, Balozi Mahiga Asema Serikali imesikitishwa na Kusitishwa kwa Msaada wa Mabilioni ya Marekani.Fahamu zaidi hapa.

Serikali imeeleza kusikitishwa na uamuzi wa Marekani kusitisha uhusiano katika Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), bila kuishirikisha wala kuisikiliza.

Kadhalika, imesema hakuna umuhimu wa misaada ya afya na elimu inayofadhiliwa na Marekani kwa dola za Marekani milioni 700 (Sh. trilioni 1.5), kama imejitoa katika kusaidia miradi ya umeme ambayo ni muhimu katika utekelezaji wa miradi inayofadhili, kwa kuwa ni sawa na kutoa kwa mkono wa kulia na kupora kwa mkono wa kushoto.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea taarifa ya uamuzi wa MCC, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga, alisema uhusiano na Marekani utaendelea katika maeneo mengine, lakini kwa fedha hizo hakuna la kufanya ingawa milango iko wazi iwapo watafikiria upya.

“Fedha ni zao, uamuzi ni wao wameutoa Washington. Hatuwezi kulia kwa ajili ya hili, tutaendeleza ushirikiano katika maeneo mengine, lakini tunawaomba wafanye uchambuzi wa kigezo cha demokrasia kwa asilimia 100 kinachotumika katika misaada hiyo,” alibainisha na kuongeza:

“Wametusaidia kwa miaka mitano kwa vile tulikidhi vigezo, ila sasa tumeshindwa kimoja inafuta imani na uelewano ambao ulikuwapo kati yetu. Nishati ndiyo nyenzo ya maendeleo kwa Tanzania. Kwa sasa tunaelekeza umeme vijijini ili vijana wanaosoma bure wajisomee na hospitali zitoe huduma muda wote.”

Waziri Mahiga alisema Tanzania imetia saini mkataba wa malengo ya milenia ambayo yanakwenda sambamba na MCC, hivyo kufuta fedha hizo kwa sasa ni sawa na kuumiza mahali panapouma zaidi huku ikiwa (Marekani) kiongozi wa utawala bora, demokrasia na soko huria duniani.

Alifananisha kunyimwa fedha hizo sawa na kutoa adhabu kwa mkosaji bila kujali kuwa alipaswa kumwelimisha na kumwonya kabla ya adhabu kubwa.

“Ukichukua mizani na kuweka nyama upande huu na jiwe upande mwingine, ukapima mazuri ambayo Tanzania imekuwa ikifanya na kuonekana mtoto mzuri machoni mwa dunia, lakini upungufu wa sasa waliouona, utaona tuna mazuri mengi, hivyo  hatukustahili adhabu hii,” alisisitiza.

“Uamuzi wao hatuwezi kuwaingilia, nasi tukiamua yetu wasituingilie. Tumejitahidi tuwezavyo kulinda demokrasia na hatutarudi nyuma kwani katika uchaguzi wa Zanzibar vyama vilishirikishwa. Waelewe na kutambua mazuri yetu tunayofanya na tutaendelea kufanya,” afafanua.

Aidha, alisema suala la Zanzibar liliendeshwa vizuri kwa kuwa lilitoa nafasi ya mazunguzo kwa pande zote na kwamba hakuna mwenye uwezo wa kuingilia masuala ya uchaguzi, serikali na mambo ya ndani ya visiwa hivyo kwa kuwa wana katiba na sheria zao bali mambo machache tunashirikiana na hata Rais Dk. John Magufuli, alikuwa mwangalizi tu.

Balozi Mahiga aliishangaa Marekani kwa kueleza kuwa uamuzi wa sasa unapingana na tamko la hivi karibuni lililosisitiza mazungumzo baada ya serikali mpya kuingia madarakani, kwa kuwa kabla ya utekelezaji, imetoa uamuzi wa kuvunja uhusiano na Tanzania katika MCC.

“Kitu kinachoitwa demokrasia kingekuwa kinafugwa kwenye bomba na kuona kinamiminika ingekuwa rahisi sana, lakini ni kitu cha kulea na kutengeneza. Tanzania imejulikana duniani kama mlezi na mjenzi wa demokrasia tangu kipindi cha chama kimoja hadi vyama vingi,” alisema.

Aidha, alisema kutokana na hali hiyo, serikali itafanya marekebisho katika bajeti yake na mpango wa maendeleo ambao ulijumuisha fedha hizo na kwamba kinachopaswa kufanyika kwa sasa ni kujikita kwenye ukusanyaji wa kodi kikamilifu.

“Ndani ya vikao vya Bunge la Marekani tuna marafiki zetu ambao tunaamini wataendelea kuihoji serikali yao juu ya uamuzi huu na hasa wakizingatia historia yetu katika kukuza na kuendeleza demokrasia nchini,” alibainisha.

Sunday, 27 March 2016

Profesa Jay Afunguka Kuhusu Chid Benz.Fahamu zaidi hapa.

Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ (pichani) amesema hali ya Mbongo Fleva, Rashid Abdallah Makwiro (31) ‘Chid Benz’ ni matokeo ya matumizi yaliyobebea ya madawa ya kulevya ‘unga’, Amani lina mchirizi wake.
 Hivi karibuni, Chid Benz aliripotiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii akionekana na hali isiyoridhisha kiasi kwamba, baadhi ya wachangiaji walisema; inauma sana!
Mwonekano wa sasa wa Chid ni wembamba wenye maswali mengi huku marafiki zake wa karibu wakidai kwamba ‘unga’ umemfanya afikie hali hiyo.
Akizungumza na gazeti hili juzi Jumanne jijini Dar baada ya kuombwa mchango wake kuhusu hali ya Chid, mbunge huyo alisema:
“Hili ni tatizo sana kwa sasa. Si kwa Chid Benz tu, bali kwa vijana wengi sana wa nchi hii ambao ni nguvu kazi ya taifa hili. Tusiwanyanyapae wale wanaoathirika na madawa bali tuwasaidie tunavyoweza ili warudi kwenye hali zao za kawaida.
“Naomba sana serikali ilichukulie suala la madawa ya kulevya kama janga kubwa sana na ilikimee kwa nguvu zote na kuweka sheria na adhabu kali ili kulinusuru taifa hili linalopoteza nguvu kazi kubwa kwa madawa ya kulevya.”
Jumatatu iliyopita, Amani lilimsaka Chid mwenyewe ili kuweza kuzungumza naye kuhusu hali yake lakini mara zote alionesha kutokuwa na utayari wa kukutana na gazeti hili hata pale gazeti lilipowatumia watu wake wa karibu, akiwemo Mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Kalama Masoud ‘Kalapina’.
Akizungumza na Amani juzi kuhusu watu walioathirika na unga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alisema wale ambao vipimo vinaonesha wameathirika, wajitokeze wakatibiwe kuondoa madhara mwilini, lakini serikali inaendelea kuwakamata wasambazaji wa biashara hiyo haramu.
“Serikali inafanya juu chini kuikomesha biashara hiyo. Kuhusu kuwakamata watumiaji, kunataka uhakika. Inawezekana mtu alitumia muda mrefu akaathirika, hao waende wakatibiwe tu ili kuondoka athari,” alisema Masauni…
KUMBUKUMBU ILIYOPITA
Oktoba mwaka 2014, Chid Benz alifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar akikabiliwa na mashtaka matatu, likiwemo la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1, 720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo, kijiko na kigae.
Chid Benz alisomewa mashtaka yake saa 7:50 mchana na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo.
Wakili Mwanaamina alisema Chid alinaswa na mzigo huo Oktoba 24, mwaka huo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Ilala jijini Dar es Salaam.
Februari mwaka jana, Chid alipatikana na hatia ambapo Hakimu Lema alimhukumu kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh. 900,000 ambapo aliweza kulipa kiasi hicho na kuwa huru.
Chanzo: GPL

Dogo Janja amchana Young Dee, Amwambia asilete uteja wake kwenye picha za watu.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya diss za mtandaoni hatimaye dogo janja amefunguka wazi kuchukizwa na kitendo cha rapa Young dee kudiss post ya Babu tale kuhusu chid benz akimtaka young dee kuacha kuleta #Uteja wake kwenye issue za watu.
Akizungumza na planetbongo dogo janja amesema amechukizwa na kukerwa kitendo cha young dee cha kudiss video ya babu tale iliyoelezea uamuzi wake wa kumsaidia chidi benz ambaye ameathirika na Dawa za kulevya akihoji kwanini young dee alidiss kitendo cha msanii mwenzake kusaidiwa.

Amesema watu wengi walianza kupost picha nyingi za kumdhalilisha chid benz kwa jinsi alivyodhohofika(baada ya kufanya interview ya kwanza na east africa radio)na hakusikia young dee akidiss kuhusu hilo lakini anashangazwa alipodiss video iliyowaonyesha mashabiki na watu wengine kuwa sasa chid benz amepata usaidizi.

Ameongeza kuwa young dee alipaswa kujua mbali na babu tale kuwa meneja lakini pia anaweza kuwa mzazi wake kwahiyo hakupaswa kumdiss kwenye mtandao kama alivyofanya. "Mtu asilete uteja wake kwenye picha za watu"alisema dogo janja.

Teja ni mtu anayetumia dawa za kulevya na dogo janja kwenye post yake instagramme kuhusu young dee lilionekana neno "Young wa kupenga" ambalo kwa maana ya mtaani mtu wa kupenga linamaanisha mtu anayetumia #unga Ambaye mara nyingi hufanya ishara hiyo muda mwingi popote.

Young dee amekuwa akiandamwa na kashfa ya kutumia Dawa za kulevya jambo ambalo mara zote amelikanusha vikali.

Aliwahi kunukuliwa akisema mtu anayetumia unga hajifichi ipo siku itafahamika kwa hiyo watu wasubiri kama ni kweli anatumia itafahamika.
-PlanetBongo

Polisi Wavamia Nyumba ya Davido Marekani...Mashabiki Wamuokoa Asikamatwe.Fahamu zaidi hapa.

Mkali wa muziki nchini Nigeria, David Adeleke ‘Davido’, amedai kwamba kutokukamatwa kwake na polisi kumetokana na mashabiki wake.

Wiki iliyopita, Davido alikuwa kwenye nyumba yake nchini Marekani, lakini polisi walikuwa na wasi wasi na msanii huyo kumiliki nyumba hiyo kwa kuwa walikuwa hawamjui kama yeye ni msanii.

“Niwe muwazi, mashabiki wangu wamenisaidia baada ya kukamatwa na polisi kwa sababu namiliki nyumba ya thamani kubwa wakitaka kufahamu ninakopata fedha.

“Ilikuwa ngumu kunielewa lakini walikuja kukubali baada ya kuwaonyesha idadi kubwa ya mashabiki zaidi ya milioni 100 wanaofuatilia kazi zangu kupitia mtandao wa ‘You Tube’.

“Nawashukuru sana mashabiki wangu nawapenda sana na nitaendelea kuwapenda katika maisha yangu,” aliandika Davido kwenye mtandao wa Instagram

DOGO JANJA AWAPA ZAWADI YA GARI WAZAZI WAKE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Baada ya Dogo Janja kununuliwa gari mpya aina ya Mercedes Benz na bosi wake Madee na kumfanya kuwa na magari mawili, amedai gari lake la zamani anawapelekea wazazi wake.


Hii ndio gari yake ya zamani ambayo amedai anaipeleka kwa wazazi wake
Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Dogo Janja alisema kwa sasa hawezi kumiliki magari mawili hivyo gari lake la zamani analipeleka kwa wazazi wake.
“Sasa hivi na magari mawili ila ile gari ya zamani itaenda nyumbani kwa wazee ili na wao wakakimbize,” alisema Dogo Janja.
Rapa huyo kwa sasa anafanya vizuri na video yake ya wimbo My Life.