Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco
(54) amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu
ya kuishi na kufanya kazi nchini bila kuwa na kibali.
Mwendesha Mashtaka wa Uhamiaji, Novatus Mlay alimemsomea mashtaka hayo leo Jumatano kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.
Akisoma hati ya mashtaka, Mlay alidai kuwa Mei 19, 2017 huko
Kinondoni katika ofisi ya uhamiaji, Marco akiwa raia wa Burundi
alikutwa nchini bila kuwa na kibali cha kumuwezesha kuishi.
Marco katika shtaka la pili amedaiwa kuwa siku hiyo alikutwa akifanya
kazi kama Mwanasheria Mkuu wa TBS bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu
kufanya kazi hapa nchini.
Katika shtaka la tatu, Mlay alidai kuwa, Julai 6 mwaka 2011 katika ofisi
ya Uhamiaji ya Dar es Salaam iliyopo Wilaya ya Ilala, mshtakiwa huyo
akiwa raia wa Burundi alitoa taarifa za uongo kuhusu maelezo yake
binafsi wakati akijaza fomu ya kuomba hati ya kusafiria namba CT
(5)(Ai).
Wakili Mlay alisema kitendo hicho cha kutoa taarifa za uongo
kilimuwezesha Marco kupata hati ya kusafiria ya Tanzania yenye namba AB
474856 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila
mmoja atasaini bondi ya Sh 20 milioni na alikamilisha. Kesi imeahirishwa
hadi Juni 21, 2017 kwa ajili ya kutajwa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment