Baada ya kutoonekana katika maandamano ya kupinga filamu za nje, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameamua kuweka wazi juu ya kundi jipya alilolianzisha.
Steve ameeleza kuwa “niliamua kujitenga na baadhi ya wasanii wenzangu wa
Bongo Muvi kwa sababu siwezi kukaa nao ndiyo maana nimeamua kuanzisha
kundi langu la watu wenye akili wanaoweza kufanya mambo ya maana na
kuleta mafanikio”.
Mchekeshaji huyo alizungumza maneno hayo na gazeti la Wikienda, na
kusisitiza kuwa angeendelea kujumuika na waigizaji hao basi angekuwa
mjinga kama wao.
“Kwanza mimi ndiye maarufu kuliko wao maana nina kipaji cha kuzaliwa,
lakini wao wamejifunza, maisha yangu ni mazuri tofauti na wao ambao hata
milioni tatu kwao kupata ni shida,” amesema Steve.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment