Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm limetangaza Msako mkali kuanzia jumatatu ijayo kwa wafanyabiashara na wauzaji wa television,Computer na simu za Mkononi zilizotumika maarufu Used’ baada ya kubaini katk maduka hayo kumekuwa maficho ya mali zinazoibiwa katika maeneo mbali mbali jijini dsm.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm Kaimu Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dsm Lucas Mkondya amesema katika miezi ya hivi karibu kumeibuka wizi wa Uvunjaji majumbani ambao wahalifu huchuku Tv hasa zile Flat screen ambapo jeshi hilo limebaini hupelekwa katika maduka hayo.
Jeshi hilo pia litawakamata watu wote wanaoendesha biashara ya magari yasiokuwa katika yard katika maeneo ya jiji la Dsm.
Aidha jeshi hilo pia kuanzia jumatatu litaendesha Msako wa Kukamata magari yote yenye Vioo vyeusi maarufu TINTED baada ya kubaini kuwa baadhi ya wahusika hujihusisha na Uhalifu na Uporaji,kuficha mali za wizi lakini pia kufanyia vitendo visivyofaa vya Uzinzi.
Akizungumzia matukio ya Uhalifu amesema watu wawili wanaosadikiwa ni majambazi wakiwa katika pikipiki eneo la upanga walimvamia na kupora kiasi cha milion 10 raia wa kihindi ambapo katika purukushani jambazi mmoja alikimbia huku aliyekuwa na bastora alidhibitiwa na kuuwawa na wananchi.
Aidha katika kutekeleza agizo la jeshi la polisi kwa majambazi waliohukumiwa na kutoka jela kujisalimisha polisi ili kujua shughuli zao,majambazi 24 wamejisalimisha huku 14 wametakiwa kujisalimisha au kusakwa na jeshi hilo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment