Monday, 31 August 2015
#YALIYOJIRI>>BANK OF AFRIKA TANZANIA YAKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 210 KUSAIDIA MATIBABU YA WATOTO WANAOZALIWA NA MIGUU ILIYOPINDA.Fahamu zaidi hapa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bank of Africa nchini Bw. Ammishadai Owusu-Amoah akimkabidhi
Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT mfano wa hundi wenye ya dola
za kimarekani 100,000 kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na
miguu iliyopinda. Nyuma ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali
Hassani Mwinyi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bank of Afrika Mwanaidi Majaar.
Balozi
Mwanaidi Majaar,Mwenyekiti wa Bodi Bank of Afrika akihutubia wadau
mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo. Balazo anasema BOA wamejizatiti
kurudisha kwa jamii wanayoihudumia na harambee ya kutibu watoto
wanaozaliwa na miguu iliyopinda ni moja ya mafanikia ya taratibu wao.
Matembezi
ya hisani ya pamoja yaliyoandaliwa na BOA na CCBRT hospitali kutoka
Leaders clup mpaka CCBRT kuadhimisha kilele cha uchangiaji wa fedha kwa
ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda.
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akihutibia na kupongeza
kwa dhati juhudi zilizofanya na zinazoendelea kufanywa na Bank of Africa kwa kujali jamii na kuhusia wadau wengine pia kuiga mfano wa BOA
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akimsalimia mtoto aliyeshiriki katika matembezi hayo.
Matembezi ya hisani
kuadhimisha kilele cha ukusanyaji fedha yakiendelea kueleka hospital ya
CCBRT.
RAIS wa Awamu ya Pili, Ali Hssan Mwinyi, jana
aliongoza matembezi ya hisani ya
kilometa tatu kutoka Leaders Club, Kinondoni hadi Hospitali ya CCBRT Msasani
kwa ajili ya kuchangia matibabu ya
watoto waliopinda miguu.
Matembezi hayo yaliyodhaminiawa na Benki ya Afrika - Tanzania, lengo kuu
lilikuwa ni kukusanya dola za marekani laki moja kwa madhumuni ya kugharamia
watoto wenye miguu iliyopinda nchini kote. Ilikuwa ni kilele cha kampeni
ya ukusanyaji wa dola za Marekani laki moja
iliyozinduliwa mwezi Aprili mwaka huu.
Kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha CCBRT kutoa matibabu ya gharama nafuu kwa
watoto 400 wenye ugonjwa wa kupinda miguu
nchini kote,ilikuyabadili maisha yao na kuwa
ya kawaida.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo jana,Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Benki ya Afrika –
Tanzania, Mwanaidi Maajar, alisema: “Benki ya Afrika – Tanzania imedhamiria
kurejesha kwa jamii kile inachopata kwa kuwa inaendesha shughuli
zake, kwa kuchangia mahitaji mbalimbali ya jamii husika. Tumeona umhimu
wa kuhimiza usaidizi katika suala hili
jema, kwa kuwa CCBRT inatoahuduma kawa
jamii maskini kwa kuondoa vikwazo mbalimbali ili jamii husika iweze kupata
matibabu,” alisema Mwanaidi .
Aidha , Ofisa Mendaji mkuu wa CCBRT,Erwin Telemans alisisitiza:
“ CCBRT inatoa shukrani za pekee kwa
Benki ya Afrika –Tanzania kutokana na ukarimu wao katika kipindi
chote cha kampeni hii. Maisha ya a mamia ya
watoto wenye ugonjwa wa kupinda miguu watapona kwa uhakika kutokana na
matibabu watakayopatiwa na CCBRT, na hatutaweza kuya badili maisha ya watoto hao bila kupata msaada kutoka kwa washirika wetu
wakarimu kama Benki ya Afrika – Tanzania.”
#YALIYOJIRI>>RAIS KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KIMBAU MAFIA.Fahamu zaidi hapa.
Baadhi
ya wanajeshi wakiwa wamebeba jeneza la Marehemu Kanali Mstaafu Ayub
Kimbau aliyewahi kuwa mbunge wa Mafia wakati wa Mazishi yake huko Kilwa
leo jioni.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la aliyewahi
kuwa Mbunge wa Mafia Kanali Mstaafu Marehemu Ayub Kimbau huko Mafia leo
jioni.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo na
watoto wa marehemu Kanali Mstaafu Marehemu Ayub Kimbau wakiomba dua
wakati wa mazishi ya Mbunge huyo wa Zamani wa Mafia yaliyofanyika huko
Mafia leo jioni.
Rais
Dkt.Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma(aliyeketi na mke wa Marehemu
kushoto) wakimfariji mke wa Marehemu Kanali Mstaafu Nyumbani Kwake Mafia
wakati wa mazishi ya Mbunge huyo wa zamani wa Mafia leo jioni.
#YALIYOJIRI>>>DC PAUL MAKONDA AZINDUA VITABU VYA MWL.LILIAN NDEGI.Fahamu hapa.
Mh.Paul Makonda akizindua vitabu
Mh.Paul Makonda alipokuwa akionesha vitabu baada ya kuzindua
Apostle Ndegi akimlisha keki Mwl Lilian Ndegi ambaye ni mke wake ikiwa ni ishara ya kupongezana.
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda alipokuwa akizungumza baada ya kuzindua vitabu.
TANGAZO KWA UMMA:JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAITA KWENYE USAILI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIARPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572 S. L. P. 260,
Fax - +255252503734 MBEYA.
TANGAZO KWA UMMA.
JESHI
LA POLISI TANZANIA LINAWAITA KWENYE USAILI WAHITIMU WALIOORODHESHWA WA
SHAHADA, STASHAHADA NA ASTASHAHADA. USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE
03.09.2015 HADI TAREHE 04.09.2015 KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA
KUMI JIONI KATIKA MAENEO YAFUATAYO:-
· FANI
YA UTAWALA, UCHUMI, USIMAMIZI WA SHERIA NA UTEKELEZAJI [BALE], UALIMU,
UANDISHI HABARI, UHANDISI MADINI [MINING ENGINEERING], UGAVI, LUGHA,
USHAURI NASIHI, KATIBU MUKTASI, LAND SURVEY CATHOGRAPHER NA GEOMATICS
WATAFANYA USAILI KATIKA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM [DPA]
KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI JIJINI DAR ES
SALAAM.
· MAFUNDI
MAGARI, MATENGENEZO YA PIKIPIKI, MAFUNDI MATENGENEZO YA UMEME WA MAGARI
[AUTO ELECTRICAL], MAFUNDI RANGI ZA MAGARI, MAFUNDI MAGARI, MAFUNDI
USHONAJI,MAFUNDI BODY ZA MAGARI NA MADEREVA. USAILI WA KADA HIZI
UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UFUNDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA
KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
· MATENGENEZO
YA KOMPYUTA, FAX & PHOTOCOPY MACHINES NA MAWASILIANO YA REDIO
[DIPLOMA IN RADIO COMMUNICATION], USAILI WAO UTAFANYIKA NYUMA YA KIKOSI
CHA UFUNDI YAANI TEHAMA KEKO CHINI.
· WAKEMIA,
BAILOJIA [MOLECULAR BIOLOGY] USAILI UTAFANYIKA MAKAO MAKUU YA POLISI
YALIYOPO MAKUTANO YA BARABARA YA OHIO NA GHANA JENGO LINALOTAZAMANA NA
POSTA HOUSE.
· KADA ZA AFYA USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA AFYA KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
· MANAHODHA
NA MAFUNDI MITAMBO WA MELI, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA
WANAMAJI KILICHOPO KARIBU NA JENGO LA MAHAKAMA YA RUFAA.
· DAKTARI
WA WANYAMA, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA MBWA NA FARASI
KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
· MAFUNDI
AC ZA MAJUMBANI, ARCHITECTURE DRAFTMAN, QUANTITY SURVEYORS, CIVIL
ENGINEER, WELDING & FABRICATION, UMEME WA MAJUMBANI, PAINTING,
ALUMINIUM & GLASS WORK, PLUMBING, MOSONRY, MOTOR REWINDING, HYDRO
GEOLOGY DRILLING WELL, REFRIGERATION & AIR CONDITIONING. USAILI WA
KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UJENZI NDANI YA KAMBI YA POLISI
BARRACKS KURASINI KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES
SALAAM.
· FANI
ZA BENDI, BRASS BENDI, WOODWIND, STRING JAZZ NA PERCUSSIVE, USAILI WAO
UTAFANYIKA KIKOSI CHA BENDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA
KURASINI DAR ES SALAAM.
· FANI YA URUBANI,USAILI UTAFANYIKA KIKOSI CHA ANGA KILICHOPO UWANJA WA NDEGE NDOGO WA ZAMANI WA J.K.NYERERE DSM.
MUHIMU:
1. MWOMBAJI
AFIKE KWENYE USAILI AKIWA NA NAKALA HALISI YA VYETI VYOTE VYA
MASOMO/TAALUMA [ACADEMIC TRANSCRIPT (S)/CERTIFICATE (S) YAANI KIDATO CHA
NNE, SITA, CHUO NA CHETI CHA KUZALIWA. KIAPO CHA KUZALIWA
HAITAKUBALIWA.
2. MWOMBAJI
ALIYEITWA KWENYE USAILI ATALIPIA GHARAMA ZA UPIMAJI AFYA SHILINGI ELFU
KUMI (10,000/=), USAFIRI, CHAKULA NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA
USAILI.
3. AMBAYE HATAHUDHURIA USAILI KUANZIA SIKU YA KWANZA HATAPOKELEWA.
ILI KUPATA/KUONA ORODHA YA MAJINA, TEMBELEA www.policeforce.go.tz
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
#YALIYOJIRI>>>Zantel yaingia ubia na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kutoa huduma za kibenki kupitia simu za mkononi.Fahamu zaidi hapa.
Waziri wa Fedha wa
Zanzibar, Mheshimiwa Omari Yusuf Mzee, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa
huduma ya Benki yako Kiganjani ya Zantel pamoja na benki ya PBZ. Kutoka kushoto
ni Mkurugenzi wa Zantel, Pratap Ghose, akifuatiwa na Mwenyekiti wa bodi ya
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Salmin Senga, na mwisho kulia ni Mkurugenzi wa
benki ya PBZ, Juma Mohammed.
Mkurugenzi wa Zantel,
Pratap Ghose akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya kati ya kampuni yake
na benki ya PBZ, Benki Yako Kiganjani.
Mkurugenzi wa Huduma ya Kifedha
za simu za mtandao, Hashim Mkudi akielezea namna ya kutumia huduma ya Benki
Kiganjani Mwako iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa kampuni yake na benki ya PBZ.
Mkurugenzi wa benki ya PBZ,
Juma Mohammed akizungumza wakati wa kuzindua huduma ya Benki Kiganjani Mwako,
inayoendeshwa na kwa ushirikiano wa benki yake na kampuni ya Zantel.
#YALIYOJIRI>>>HOTUBA YA MHESHIMIWA PROF. MAKAME M. MBARAWA (MB), WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA WAANDISHI WA HABARI YA KUTANGAZA RASMI KUANZA KUTUMIKA KWA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO NA YA MIAMALA YA KIELEKTRONIKI ZA MWAKA 2015 KWENYE UKUMBI WA MIKUTANO WA WIZARA TAREHE 31 AGOSTI, 2015.Fahamu zaidi hapa.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (Mb), akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuanza kutumika rasmi kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao na ya Miamala ya Kieletroniki za mwaka
2015. Anayeangalia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bwana John Mngodo.
Hawa ni waandishi wa habari wakati wa mkutano na wahandishi wa habari kuusu kuanza kutumia rasmi kwa sheria ya Makosa ya Mitandao na ya Miamala ya Kieletroniki za Mwaka 2015.
Ndugu Wandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana,
Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru nyote hasa waandishi wa habari kwa kutenga muda wenu na kujumuika nasi kwa lengo la kutangaza rasmi kuanza kutumika kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 ambayo ilitangazwa kwenye gazeti la Serikali la tarehe 14/08/2015 na kupewa Na. 328. Pia Sheria ya Miamala ya Kielektroniki, 2015 ambayo ilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe hiyo hiyo na kupewa Na.329.
Ndugu Wananchi,
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni nyenzo ya kisasa inayotumika kubeba na kusafirisha ujumbe, taarifa, takwimu, picha na sauti kwa kutumia njia na mifumo mbalimbali ya mawasiliano iliyopo, kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine au eneo moja kwenda eneo lingine kwa uharaka, ufasaha, kwa wakati na kwa kiwango cha ubora ule ule bila kujali umbali na mipaka iliyopo ya kijiografia. Matumizi ya TEHAMA yameleta mafanikio katika kuharakisha, kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia kukuza uchumi na kuleta maendeleo nchini. Mathalani, wananchi walio wengi sasa wanapata huduma mbalimbali za kifedha, kulipia huduma (leseni, kodi, Ankara), matumizi ya mitandao ya kijamii, barua pepe na huduma mtandao kama vile Serikali mtandao, afya mtandao, kilimo mtandao, biashara mtandao, Elimu mtandao, n.k
Ndugu Wananchi
Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo kumekuwepo na changamoto mbalimbali kama vile wizi wa fedha kwa njia ya mtandao, uvujaji wa taarifa, kusambazwa kwa ujumbe wa matusi, picha chafu, uchochezi, udhalilishaji, vitisho kupitia mitandaoni. Vile vile kuna watu wachache ambao wanaharibu miundombinu ya mawasiliano, kwa mfano wanakata mkongo wa Taifa wa mawasiliano na mikongo mingine ya mawasiliano na hili lina athari kubwa sana kwa nchi yetu na kwa nchi za jirani ambazo zimeunganishwa kwenye mkongo wa Taifa wa mawasiliano.
Ndugu Wananchi
Mtakumbuka kuwa, mnamo tarehe 1 Aprili 2015 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya Mwaka 2015. Pamoja na masuala mengine, sheria hizi zinabainisha makosa, kutambua ushahidi wa nyaraka za kielektroniki na pia kuainisha adhabu zinazokwenda pamoja na makosa mbalimbali ya kimtandao. Sheria hizi ni muhimu sana na zina manufaa makubwa kwenye jamii yetu haswa katika nyakati hizi ambapo matukio ya uhalifu wa mtandao yamekuwa yakiongezeka na kukosekana kwa Sheria hizi kumefanya Wananchi kutokuwa na mahala pa kukimbilia pale wanapokumbana na uhalifu kupitia mitandaoni.
Aidha, ninatambua ya kuwa Sheria hizi zimepokelewa kwa hisia tofauti kutokana na uelewa mdogo kwa wengi wetu kuhusu sheria hizi. Vilevile ni ukweli usiopingika kuwa kumekuwa na tafsiri hasi kwa baadhi ya wananchi juu ya maudhui ya sheria hizi na kuzifanya zitafsiriwe kama kandamizi zaidi kitu ambacho ni tofauti na dhana na maudhi ya sheria hizi.
Kwa kutambua hilo, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia mara baada ya kupitishwa kwa SHERIA hizi ilianza kuwaelimisha wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari na kuwa na mikutano na makundi mbalimbali ya watekelezaji wa Sheria hizi ili kuwajengea uelewa ikiwemo Jeshi la Polisi, Waendesha Mashtaka, Wachunguzi, Wapelelezi, Mahakimu na Majaji kuhusu Sheria hizi kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani Bara na Zanzibar. Aidha, ili kuhakikisha kuwa usimamizi na utekelezaji wa Sheria hizi unakwenda vizuri, Wizara itaendelea kuwajengea uelewa Wadau mbalimbali.
Ndugu Wananchi
Tanzania siyo nchi ya kwanza kutunga sheria kama hizi. Kuna nchi mbalimbali duniani ambazo zimetunga sheria kama hizi, kwa mfano nchi ya Uingereza (UK Computer Misuse Act, 1990), India (IT Act, 2000), Malaysia (Computer Crime Act), Uganda (Computer Misuse Act, 2010), Korea ya Kusini (Information and Communications Network Act na Information and Communication Infrastructure Protection Act), Singapore (The Computer Misuse and Cyber security Act), Mauritius (Computer Misuse and Cybercrime Act, 2003), Marekani (Computer Fraud and Abuse Act, 1984) na nyingi nyenginezo.
Ndugu Wananchi,
Serikali baaada ya kujiridhisha kuwa maandalizi yote muhimu ikiwemo elimu kwa umma na kujenga uelewa kwa watekeleza wa sheria hizi yamefanyika. Sasa, Sheria hizi zitaanza kutumika rasmi tarehe 01/09/2015.
Kwa hivyo, natoa rai na wito kwa wananchi wote kuwa tuzingatie “Matumizi Salama na sahihi ya Huduma za Mawasiliano na Mtandao kwa manufaa ya kila mmoja na kwa maendeleo ya Taifa letu. Mitandao ikitumiwa vema ina faida kubwa sana katika jamii yetu.
"AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA"
Toa maoni yako hapa.
#Breaking News>>>Njombe yavunja lekodi Mapokezi ya Mgombea Urais Kupitia UKAWA Edward Lowassa hii leo.Fahamu Zaidi hapa.
Mgombe Urais wa UKAWA, Mhe. Edward Lowassa akimnadi Mgombe
Ubunge Jimbo la Makambako, Mhema Oraph. Uwanja wa Polisi
Waziri Mkuu Mstaafu,FredrickSumaye akiongea jambo na Mgombea Urais UKAWA EdwardLowassa leo Njombe.
"Sheria mpya ya mitandao inaanza kesho, kuweni waangalifu " Lawrence Masha Akiwa anazungumza na Wananjombe hii leo.
Umati wa Wakazi wa Njombe Wakiwa wamebeba Msaraba
Umati wa Wakazi wa Njombe uliojitokeza kumsikiliza Mgombe Urais Mhe. Edward Lowassa hii leo.
Umati wa Wakazi wa Njombe uliojitokeza kumsikiliza Mgombe Urais Mhe. Edward Lowassa hii leo.
Umati wa Wakazi wa Njombe uliojitokeza kumsikiliza Mgombe Urais Mhe. Edward Lowassa hii leo.
Umati wa Wakazi wa Njombe uliojitokeza kumsikiliza Mgombe Urais Mhe. Edward Lowassa hii leo.
Umati wa Wakazi wa Njombe ukisubili kumpokea Mgombe Urais Mhe. Edward Lowassa hii leo.
Umati wa Wakazi wa Njombe ukisubili kumpokea Mgombe Urais Mhe. Edward Lowassa hii leo.
Msafara wa Mgombe Urais Mhe. Edward Lowassa Kupitia UKAWA Msafara wake ukiwasili
kwenye Viwanja vya Mdete Njombe mjini
Mgombe Urais wa UKAWA akiwasalimia wakazi wa Njombe hii leo.
Mgombe Urais wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na Wagombea Udiwani wa Jimbo la Njombe hii leo.
Wauza viatu wakimshangilia Mgombea Urais wa UKAWA, Mhe. Edward Lowassa.... Njombe hii leo.
Umati wa Wakazi wa Njombe uliojitokeza kumsikiliza Mgombe Urais Mhe. Edward Lowassa hii leo.
Bibi akiwa anaonyesha ishara ya Vidole Viwili kumaani Chadema Amakweli,Bibi anataka mabadiliko hii imetokea hii leo huko Njombe.
Umati wa Wakazi wa Njombe ukisubili kumpokea Mgombe Urais Mhe. Edward Lowassa hii leo.
Toa maoni yako hapa.