Mbunge wa Bunda Mjini Mh. Ester Bulaya ametoa salamu kwa Wabunge wa CCM
pamoja na Spika Job Ndugai kutambua kwamba hata baada ya kumuadhibu
kutohudhuria vikao bya bunge siyo silaha ya kuwafunga midomo.
Bulaya amefunguka hayo akiwa Mkoani Kilimanjaro na kusema kwamba uamuzi
uliofanya na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Wabunge CCM
pamoja na Spika wa bunge haujawatendea haki wananchi wao kwa sababu ni
kwa muda mrefu watakosa wawakilishi bungeni ingawa siyo mwisho kwa wao
kupigania haki na kuwatumikia wananchi kwa njia zingine.
"Wamekosea sana kwa sababu wananyima wananchi wetu haki ya kupata
wawakilishi wa matatizo yao bungeni. Ingawa tayari tumekwishaweza
kujipanga namna ya kwenda kuwatumikia na kupeleka maendeleo kwa katika
kipindi hichi ambacho tutakuwa nje ya bunge. Lakini niweke wazi adhabu
hii kutolewa siyo silaha ya kutuifanya kuacha kupigania demokrasia na
haki. Bulaya alifunguka.
Aidha Bulaya ametupa lawama kwa Mh. Ndugai na kudai kuwa ni kiongozi
asiyeweza kuzuia hasira ndio maana amekuwa na maamuzi ya kuhukumu haraka
wakati yeye ni baba anayepaswa kuwa na subira na uvumilivu wa kuongoza.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment