Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za injili, Rose Muhando akituhumiwa kujipati fedha kwa njia ya udanganyifu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Debora
Mgiligimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mwimbaji
huyo alikamatwa juzi Wilaya ya Ikungi baada ya wadeni wake ambao ni
Waumini wa Kanisa la AICT Singida kupata taarifa kuwa yupo wilayani
humo.
Inadaiwa
kuwa Novemba 3 mwaka jana, mwimbaji huyo alitumiwa fedha na Mwenyekiti
wa Kwaya ya Kanisa la AICT Singida, Mashala Japhet Tsh 800,000 ambapo
zilitumwa baada ya pande mbili kukubaliana kuwa angekwenda kwenye
uzinduzi wa Album ya kwaya na kanisa hilo, hata hivyo hakutokea.
Kwa
mujibu wa kamanda huyo, uzinduzi wa kwaya hiyo ulikuwa ufanyike Novemba
13 mwaka jana, saa 8 mchana katika uwanja wa Namfua Singida.
Novemba
8 mwaka jana, mwimbaji huyo aliomba kutumiwa tena 150,000 kwa ajili ya
nauli ya kutoka Dodoma kwenda Singida yeye na wasaidizi wake, fedha
ambayo ilitumwa na mawasiliano yakaendelea kufanyika ili kuakikisha kuwa
siku ya tukio anakuwepo.
Chakushangaza,
siku ya tukio msanii huyo hakujitokeza na walipata taarifa kuwa yupo
Kahama anatoa huduma, walipofanya mahojiano walithibitisha kuwa ni
kweli.
Alipofanyiwa
mahojiano na Polisi, Rose Muhando alikiri kutenda kosa hilo kwa kutotoa
taarifa kwamba hawezi kuja na alieleza si kweli kwamba alikuwa kahama,
bali alikuwa na mgonjwa nyumbani hivyo hakuweza kutoka. Muhando amesema
kuwa yupo tayari kurejesha fedha hizo alizotumiwa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment