Tuesday 4 August 2015

#Breaking news>>>Kutoka Burundi Mwanaharakati apigwa risasi.




Mwanaharakati maarufu wa haki za kibinaadamu nchini Burundi ameigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na watu waliokuwa katika pikipiki kulingana na familia yake na watu walioshuhudia.
Pierre Claver Mbonimpa alishambuliwa katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura.Amekuwa mkosoaji mkubwa wa tangazo la rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Siku ya jumapili mshauri wa rais huyo jenerali Adolphe Nshimirimana aliuawa katika shambulizi ndani ya gari lake mjini Bujumbura.Alikuwa akisimamia usalama wa rais.
Burundi imekabiliwa na ghasia tangu hatua ya rais Nkurunziza mnamo mwezi Aprili kutaka kuwania muhula wa tatu.
Wapinzani wamedai kwamba hatua hiyo ni kinyume na katiba huku jaribio la mapinduzi likifeli mnamo mwezi Mei.
Uchaguzi wa urais ulifanyika mwezi uliopita ambapo bwana Nkurunziza alishinda lakini ulisusiwa na upinzani.
Jamaa mmoja ya bwana Mbonimpa aliambia shirika la habari la reuters kwamba mwanaharakati huyo alikuwa katika chumba kimoja cha wagonjwa mahututi katika hospitali moja ya Bujumbura kufuatia shambulio hilo lililofanyika karibu na nyumba yake kaskazini mwa mji huo.
Chanzo
             BBC

0 comments:

Post a Comment