Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisoma bango la
vijana wafanya biashara ndogo ndogo wa eneo la Dumila maarufu kama Feri
wakati akielekea mkoani Tanga ikiwa muendelezo wa mikutano ya kampeni za
CCM
Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli(katikati) akiwanadi
Mbunge wa Handeni Mjini Dk. Abdallah Kigoda (kulia) na Mgombea wa Ubunge
Jimbo la Handeni Vijijini Ndugu Mboni Mhita kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika kwenye uliofanyika kwenye uwanja wa Azimio Center.
Wakati
kampeni za kuwania Urais,Ubunge na Udiwani zikidizi kushika kasi
nchini,Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John
Pombe Magufuli,amesema atasimamia utawala wa sheria kwa kuwawajibisha
wale wote wanaopindisha sheria kwa faida yao.
Magufuli
aliyepewa jukumu la kuipeperusha bendera ya chama cha Mapinduzi,katika
ngazi ya urais,amesema utawala wake hautakuwa na simile na wanaopoka
haki za wanyonge,amesema
kuwa ni jambo lisilokubalika kuona haki za wanyonge zikipokwa na
matajiri wachache na kuelezea kuwa atawashughulikia kwa mujibu sheria
zilizopo.
Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
Turiani mkoani Morogoro na kuwaambia atahakikisha migogoro ya ardhi
inamalizika na kuileta jamii kuishi kwa amani na upendo.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa wasili
katika kijiji cha Muheza-Masagala akielekea wilayani Handeni kuwahutubia
wananchi katika mkutano wa kampeni
Baadhi
wananchi wa kijiji cha Vyadigwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt
Magufuli (hayupo pichani) alipowahutubia wakazi wa kijiji hicho wilayani
Kilindi
Tea
Magufuli ya Handeni nayo ilikuwepo kuwahamasisha wananchi wampigie kura
ya ushindi Dkt Magufuli,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
uwanja wa Kigoda.
Toa maoni yako hapa.
0 comments:
Post a Comment