=>Hatuna kipangamizi Rais kumteua yeyote
=> ACT Wazalendo ni chama cha siasa cha kutumikia wananchi
=> Rais kavunja mwiko kwa kuanza kuteua wapinzani
=>Huu ni uthibitisho kwamba ACT ina viongozi bora hivyo inaweza kuongoza nchi.
=>Bado tunao wazalendo wa kutosha, hivyo raia asisite kuchagua wengine
=>CCM wajifunze kupitia kwetu kuchagua viongozi bora
=>Kamati ya uongozi inamshauri Rais kuweka mfumo bora wa kuazima watu
kutoka vyama vingine kwa kuweka mashauliano ili kuepuka migongano ndani
ya vyama.Japo anao uwezo, hii ni kuimarisha umoja wa kitaifa
=> Kuteua bila mashauriano kunaleta wasiwasi miongoni mwao
=>ACT inampongeza Anna Mghwira kwa kuteuliwa
=> ACT imeona kutakuwa na mgongano kati ya nafasi yake na chama
=> Katiba ya ACT Wazalendo, Mama Anna Mgwhira amekoma kuwa mwenyekiti.
=> Kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa hawezi fanya kazi kwa ufanisi kwa ACT- wazalendo.
=>ACT inamshukuru kwa kufanya kazi kwa uzalendo na ACT Wazalendo imemteua ndugu Yeremia Maganja kuwa Makamu Mwenyekiti mpya
Maswali
1. Je, hamjashauriana katika uteuzi huu?
=> Kama tulivyoeleza mwanzo, Rais alimteua mama wakati yupo nje ya
nchi na sisi tulipata taarifa na tukamtafuta kwa mashauriano. Tumetoa
tamko baada ya kushauriana na Mama Mghwira
2. Mama bado ni Mwanachama halali wa ACT Wazalendo, Kupewa ilani ya CCM mnaichukuliaje?
=> Rais na vitengo vyake vyote vimejilidhisha kwamba ACT ina viongozi
waadilifu, huu ni ujumbe kwa watanzania kwamba ACT-Wazalendo ipo tayari
kupewa nchi. Na watanzania wenyewe wameona
=>Ni mujimu haya mambo yakaeleweka, tunapofanya uchaguzi, wananchi
wanasoma na kuchagua ilani ambayo wanaona inafaa. Kwa hivi sasa chama
kinachoongoza ni CCM na ilani inayotekelezwa ni ya CCM. Mwaka 2015 Mama
Anna pia alimpa ilani ya ACT Wazalendo na tunaamini kuna mambo mazuri ya
Ilani ya ACT
=>ACT tungeshinda tungeunda serikali ya umoja wa kitaifa, hivyo hiki
kinachofanywa ni moja ya Malengo tuliyokuwa nayo.ACT tungechagua watu
kutoka vyama vyote
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment