AKITUA tu nchini na kumalizana na Simba, mshambuliaji mwenye kasi na
mwendo wa kuyumba uwanjani, Emmanuel Anorld Okwi ndiye atakuwa mchezaji
ghali zaidi wa Simba.
Simba imejipanga kumalizana na Okwi kwa dau la dola 50,000 (Sh milioni
110), pia atakabidhiwa nyumba ya kuishi katika maeneo ya Sinza, Mbezi
Beach au Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba, tayari kupitia kamati ya ufundi
na ile ya usajili, wamekubaliana kuwa Okwi ndiye chaguo namba moja kwa
wachezaji wa kigeni.
Juzi, Okwi aliliambia Championi kutoka Senegal kwamba bado hawajafanya
mazungumzo “siriaz” na Simba, lakini wakikubaliana yuko tayari kuja.
Imeelezwa kwa kuwa Okwi yuko huru, yaani hana mkataba na Sports Club
Villa anayoichezea, kamati hiyo imekuwa ikipambana kuhakikisha dau hilo
linashuka angalau kufikia dola 25,000 (Sh milioni 55).
Kiongozi mwingine anayehusika na usajili alisema: “Fedha hizo ni nyingi
sana, Okwi hana mkataba na Villa, hivyo najua itapungua ili kuhakikisha
mambo yanakwenda vizuri. Simba tungependa kununua wachezaji kwa
kupunguza gharama.”
Habari kutoka ndani ya Simba tayari wanahangaika kupata fedha hizo na
tayari kiasi fulani kimepatikana tayari kumshusha Okwi Dar es Salaam.
“Kamati imepitisha na tumekubaliana, tunataka mtu wa kuamua matokeo timu
inapokuwa imezidiwa. Tunataka mtu wa kushirikiana na wenzake kumaliza
kazi na Okwi hatuna shida naye,” alisema.
Kama hiyo haitoshi, imeelezwa mmoja wa wanachama wenye nazo ndani ya
Simba, yeye ameamua kutoa gari lake ili Okwi awe analitumia wakati akiwa
Tanzania.
Mganda huyo yupo Senegal ambako timu ya taifa ya Uganda, The Cranes imeweka kambi na wikiendi hii inacheza dhidi ya Ivory Coast.
Baada ya hapo, Okwi atarejea Kampala na matumaini makubwa kuanzia
Jumatatu hadi Ijumaa, dili litakuwa limefungwa na Okwi kutangazwa rasmi
huku akirudishiwa jezi yake namba 25.
Credit - Champion
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment