Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema mtu yeyote atakayebainika amemkatisha
mwanafunzi wa kike masomo kwa kumpa mimba au kumfanyia vitendo vya
ukatili vitakavyopelekea kukatisha masomo yake ni lazima afungwe miaka
30 jela.
Majaliwa
ametoa agizo hilo leo Lugalo jeshini Jijini Dar es Salaam wakati
akizindua na kukabidhi vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye
mahitaji maalumu vyenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 16.9 kwa
ajili ya shule 1696 kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha uboreshaji
wa masomo ya sayansi.
Vilevile
Majaliwa ameiagiza TAMISEMI kuhakikisha wanakamilisha maabara za shule
zote nchini 4587 ambazo bado hazijakamilika ili vifaa hivyo vianze
kusaidia wanafunzi kwa haraka na kufikia malengo ya nchi ya kuwa ya
uchumi wa kati.
Pamoja
na hayo, Majaliwa amesema watendaji watakaoenda kinyume na maadili ya
kazi zao ni lazima mkono wa sheria uchukue nafasi yake.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment