Saturday 5 August 2017

Wakwe Wavunja Ndoa ya Mziwanda...Wamuozesha Nawal Kwa Mwanaume Mwingine Mwenye Pesa Bila Nuh Kutoa Talaka.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuh Mziwanda ambaye hivi karibuni kumeibuka minong'ono kuwa ndoa yake imesambaratika, amefunguka kuhusu hilo na kukiri kuwa kweli ndoa hiyo imekufa bila talaka, huku mke wake akiwa mbioni kuolewa na mtu mwingine.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Nuh Mziwanda amesema mke wake huyo hajampa talaka lakini ameolewa na mtu mwengine, huku vuguvugu kubwa lilianza kwa wakwe zake (wazazi wa mke wake)

Mimi na Nawal tulitengana tu, lakini baada ya hapo kumbe mwenzangu ameshaandaliwa mume wa kumuoa, mimi baada ya kugundua hilo nikaona bora nirudi kwenye dini yangu, kwa hiyo wazazi wa mke wangu walikuwa wanajua kuwa mtoto wao ananisaliti", alisema Nuh Mziwanda.

Nuh Mziwanda alipoulizwa kama alitoa talaka kwa mke wake huyo kama sheria ya ndoa inavyotaka watu wanapoachana, Nuh alisema hajatoa talaka na hawezi kutoa kwani tayari Nawal mke wa mtu.


"Mimi sijatoa talaka, na kufuatilia suala la talaka itakuwa kama najichoresha kwani wao wazazi wanajua kabisa kama ni mke wangu lakini wao wakaamua kumuozesha kwa mtu mwingine, kwa hiyo mimi naacha tu, mimi nitaangalia utaratibu wa kumlea mwanangu kwani bado mdogo hivyo bado yuko na mama yake", alisema Nuh Mziwanda.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment