Wednesday 5 August 2015

#YALIYOJIRI>>Bei mpya ya mafuta EWURA yatangaza.




Bei za mafuta ya Petrol imepanda kwa Tsh 92/lita sawa na ongezeko la 4.91% ukilinganisha na mwezi uliopita.Kwa mfano hapa Arusha mwezi uliopita mafuta ya petrol ilikua ni Tsh 2,282/lita kwa sasa bei Tsh 2,374/lita

Ni neema kwa watumiaji wa Diesel ambayo kwa mwezi huu imeshuka kwa Tsh 17.5/lita sawa na 0.9% pamoja na mafuta ya taa yalioshuka kwa Tsh 29.27/lita sawa na 1.55% ukilinganisha na mwezi uliopita.

Sababu kubwa ya upandaji wa gharama ya mafuta ni mrundikano wa bidhaa kutoka nje kwenye bandari ya Tanga pamoja na gharama za usafirishaji kutoka hapo Tanga kwenda sehemu mbalimbali za nchi.




KUMB: PPR/15 - 08/1
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI KUANZIA
JUMATANO, TAREHE 5 Agosti 2015
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 5 Agosti 2015. Pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-

                        (a) Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote yaani Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 1 Julai 2015. Kwa Mwezi Agosti 2015, bei za rejareja kwa Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kama ifuatavyo: TZS 18/lita sawa na asilimia 0.86 na TZS 29/Lita sawa na asilimia1.47 sawia,na kwa mafuta ya Petroli bei imeongezaka kwa TZS 92 /lita sawa na asilimia 4.19. Vilevile kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla kwa mafuta ya Dizeli na Mafuta ya Taa nazo zimepungua kama ifuatavyo: TZS 17.50/lita sawa na asilimia 0.90 na TZS 29.27/lita sawa na asilimia 1.55sawia na kwa mafuta ya Petroli bei imeongezeka kwa TZS 92.07/lita sawa na asilimia 4.40. Mabadiliko haya yametokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia.

                        (b) Kufuatia uamuzi wa kuanza kupokea mafuta chini ya mfumo wa BPS kupitia pia bandari ya Tanga, Mamlaka inatoa taarifa kuwa ukokotoaji wa bei za mafuta kwa wafanyabiashara watakaosambaza mafuta yatakayopokelewa kupitia bandari ya Tanga, utafanyika kwa kuzingatia gharama halisi za bandari hii na pia gharama za usafirishaji kutokea Tanga. Kwa kuanzia, kwa mwezi Agosti wilaya zote za mkoa wa Tanga zitapokea mafuta kupitia Tanga na ukokotoaji wa bei kwa wilaya hizi utazingatia hili.

                        (c) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

                        (d) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 7 la tarehe 4 Machi 2015.

                        (e) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.

2


                        (f) Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

A: BEI ZA REJAREJA
Mji
Bei Kikomo
Petroli
Dizeli
Mafuta Ya Taa
(Sh/Lita)
(Sh/lita)
(Sh/Lita)
Dar es Salaam
2,290
2,026
1,964
Arusha
2,374
2,110
2,048
Arumeru (Usa West)
2,374
2,110
2,048
Karatu
2,392
2,128
2,066
Monduli
2,379
2,115
2,053
Ngorongoro (Loliondo)
2,430
2,166
2,104
Kibaha
2,295
2,030
1,969
Bagamoyo
2,301
2,037
1,975
Kisarawe
2,297
2,033
1,971
Mkuranga
2,300
2,035
1,974
Rufiji
2,318
2,053
1,992
Dodoma
2,349
2,084
2,023
Bahi
2,356
2,092
2,030
Chemba
2,375
2,111
2,049
Kondoa
2,381
2,117
2,055
Kongwa
2,346
2,082
2,020
Mpwapwa
2,350
2,086
2,024
Iringa
2,354
2,090
2,028
Kilolo
2,358
2,094
2,032
Mufindi (Mafinga)
2,364
2,100
2,038
Njombe
2,382
2,118
2,056
Ludewa
2,420
2,156
2,094
Makete
2,413
2,149
2,087
Wanging'ombe (Igwachanya)
2,380
2,116
2,054
Bukoba
2,505
2,241
2,179
Biharamulo
2,479
2,215
2,153
Karagwe (Kayanga)
2,521
2,257
2,195
Kyerwa (Ruberwa)
2,527
2,263
2,201
Muleba
2,505
2,241
2,179

3


Ngara
2,471
2,206
2,144
Misenyi
2,513
2,249
2,187
Geita
2,455
2,191
2,129
Bukombe
2,444
2,180
2,118
Chato
2,476
2,212
2,150
Mbogwe
2,493
2,229
2,167
Nyang'hwale
2,470
2,206
2,144
Kigoma
2,521
2,257
2,195
Uvinza (Lugufu)
2,533
2,269
2,207
Buhigwe
2,510
2,246
2,184
Kakonko
2,478
2,214
2,152
Kasulu
2,507
2,243
2,181
Kibondo
2,485
2,221
2,159
Moshi
2,364
2,099
2,038
Hai (Bomang'ombe)
2,367
2,103
2,041
Mwanga
2,357
2,092
2,031
Rombo (Mkuu)
2,385
2,120
2,058
Same
2,350
2,086
2,024
Siha (Sanya Juu)
2,370
2,106
2,044
Lindi
2,349
2,084
2,023
Kilwa Masoko
2,324
2,060
1,998
Liwale
2,370
2,105
2,044
Nachingwea
2,378
2,114
2,052
Ruangwa
2,376
2,112
2,050
Babati
2,412
2,148
2,086
Hanang (Katesh)
2,423
2,158
2,097
Kiteto (Kibaya)
2,423
2,159
2,097
Mbulu
2,425
2,161
2,099
Simanjiro (Orkasumet)
2,444
2,180
2,118
Musoma
2,468
2,204
2,142
Rorya (Ingirijuu)
2,477
2,213
2,151
Bunda
2,459
2,195
2,133
Butiama
2,465
2,201
2,139
Serengeti (Mugumu)
2,514
2,249
2,188
Tarime
2,479
2,215
2,153
Mbeya
2,397
2,133
2,071
Chunya
2,406
2,142
2,080
Ileje
2,410
2,146
2,084
Kyela
2,413
2,148
2,087
Mbarali (Rujewa)
2,381
2,117
2,055
Mbozi (Vwawa)
2,406
2,142
2,080
Momba (Chitete)
2,415
2,151
2,089

4


Rungwe (Tukuyu)
2,406
2,142
2,080
Morogoro
2,315
2,051
1,989
Mikumi
2,331
2,066
2,005
Kilombero (Ifakara)
2,353
2,088
2,027
Ulanga (Mahenge)
2,363
2,099
2,037
Kilosa
2,333
2,069
2,007
Gairo
2,333
2,069
2,007
Mvomero (Wami Sokoine)
2,325
2,061
1,999
Turian
2,340
2,076
2,014
Mtwara
2,362
2,098
2,036
Nanyumbu (Mangaka)
2,411
2,147
2,085
Masasi
2,388
2,124
2,062
Newala
2,394
2,130
2,068
Tandahimba
2,387
2,123
2,061
Mwanza
2,440
2,175
2,114
Kwimba
2,476
2,212
2,150
Magu
2,448
2,184
2,122
Misungwi
2,445
2,181
2,119
Sengerema
2,472
2,208
2,146
Ukerewe
2,499
2,235
2,173
Sumbawanga
2,463
2,198
2,136
Kalambo (Matai)
2,455
2,191
2,129
Nkasi (Namanyele)
2,476
2,212
2,150
Katavi (Mpanda)
2,498
2,233
2,171
Mlele (Inyonga)
2,476
2,212
2,150
Songea
2,413
2,149
2,087
Mbinga
2,447
2,182
2,121
Namtumbo
2,442
2,178
2,116
Nyasa (Mbamba Bay)
2,449
2,185
2,123
Tunduru
2,472
2,208
2,146
Shinyanga
2,419
2,154
2,093
Kahama
2,432
2,168
2,106
Kishapu
2,447
2,183
2,121
Simiyu (Bariadi)
2,460
2,196
2,134
Busega (Nyashimo)
2,453
2,189
2,127
Itilima (Lagangabilili)
2,463
2,199
2,137
Maswa
2,451
2,187
2,125
Meatu (Mwanhuzi)
2,459
2,194
2,132
Singida
2,381
2,116
2,054
Iramba
2,393
2,128
2,067
Manyoni
2,365
2,101
2,039

5


Ikungi
2,376
2,112
2,050
Mkalama (Nduguti)
2,405
2,141
2,079
Tabora
2,444
2,180
2,118
Igunga
2,398
2,134
2,072
Kaliua
2,462
2,198
2,136
Ulyankulu
2,456
2,192
2,130
Nzega
2,409
2,144
2,082
Sikonge
2,456
2,191
2,130
Urambo
2,457
2,193
2,131
Tanga
2,277
2,010
2,010
Handeni
2,298
2,031
1,989
Kilindi
2,313
2,046
2,024
Korogwe
2,289
2,022
2,003
Lushoto
2,299
2,032
2,013
Mkinga (Maramba)
2,284
2,017
2,024
Muheza
2,282
2,015
2,010
Pangani
2,284
2,017
2,017

B: BEI ZA JUMLA
Bei za Jumla - DSM
Petroli (Sh/L)
Dizeli (Sh/L)
Mafuta ya Taa (Sh/L)
Bei Kikomo
2,185.10
1,920.74
1,858.99

Bei za Jumla - TANGA
Petroli (Sh/L)
Dizeli (Sh/L)
Bei Kikomo
2,172.32
1,905.25

Felix Ngamlagosi
MKURUGENZI MKUU
EWURA

 

0 comments:

Post a Comment