Imeelezwa
kuwa sekta binafsi zimetajwa kuwa na mchango mkubwa katika harakati za seriklai
za kupambana na tatizo la rushwa amabalo limekuwa likiathiri shughuli za
kimaendeleo hapa nchini.
Hayo
yameelezwa na rais Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya kutia saini hati tatu za
maadili ambapo amesema licha ya baadhi ya watendaji katika sekta ya umma
kulalamikiwa katika suala la rushwa sekta binafsi zinaweza kuisadia serikali
katika kukabiliana natatizo hilo.
Waziri
wa nchi ofisi ya rais utawala bora George Mkuchika amewasisitiza watendaji
katika sekta ya umma kuhakikisha wanatekeleza ahadi za viapo hivyo vya maadili
nakwamba maadili yatakuwa ni moja ya kigezo katika ajira yoyote serikali huku
akisisitiza kuanza kufanya kazi muda mfupi baada ya kusainiwa na rais.
Licha
ya kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini, sekta binafsi inasema
ni vema sekali ikajitahidi kushughulikia rushwa kwani kwa kiasi kikubwa imekuwa
ikiathiri utendaji wao wa kazi hasa kwa wawekezaji.
Hati
hizo tatu zilizosainiwa ni pamoja na hati ya ahadi ya maadili kwa viongozi wa
umma, hati ya ahadi ya maadili kwa watumishi wa umma na hati ya ahadi ya
maadili kwa sekta binafsi.
Hafla
hiyo ya utiaji saini ahadi za maadili imefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na
kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wandamizi serikalini ambapo kwa mujibu wa
tume ya maadili utekelezaji wake tayari umekwisha kuanza.
Chanzo
ITV HABARI.
0 comments:
Post a Comment