Monday, 7 September 2015

#YALIYOJIRI>>>ZOEZI LA KUWAPOKEA WAKIMBIZI KUTOKA BURUNDI LAENDELEA VIZURI KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU MKOANI KIGOMA.Fahamu zaidi hapa.

 Mkuu wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Fredrick Nisajile akiongea na wakimbizi walio katika mpango wa kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Mtendeli na Karago.Wakimbizi hao waliopokelewa kutoka nchini Burundi hivi karibuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa muda katika kambi ya Nyarugusu.
 Wakimbizi kutoka nchini Burundi wakipanga mizigo yao katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wamehifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli ikiwa ni mkakati unaoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengine ya kimataifa ili kuwapatia makazi salama.
  Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Kukimana Dafroza (katikati), akifuma kikapu kama alivyokutwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa katika kambi nyingine. Wengine ni Mkabanura Eviline (kushoto) na Niragira Dafroza (kulia).
  Mkimbizi Joseph Mtagura aliyeko katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu akiandaa mihogo ya kuwauzia wakimbizi wenzake wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma
 Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wakichota maji jana katika moja ya vituo vya maji vilivyowekwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda.  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ina mpango wa kuwahamishiwa katika kambi za Karago, Mtendeli na Nduta ili kupunguza msongamano uliopo katika Kambi ya Nyarugusu.
 Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Jacqueline Elulu (mwenye mtoto), akisubiri kupata huduma ya afya katika kituo cha Red Cross kinachotoa huduma za afya kwa wakimbizi walioko katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Shirika la Red Cross ni mojawapo ya wadau wanaoshirikiana na Serikali kutoa huduma za afya katika kambi ya Nyarugusu.
 Wakimbizi kutoka Burundi walioko katika Kambi ya Nyarugusu wakiandaa mboga ya kisamvu kama walivyokutwa na mpiga picha wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeko katika ziara  katika kambi hiyo.

Mkimbizi Haverimana Ejide (kushoto) na mkewe Kugimana Evona pamoja na watoto wao wakipata chakula cha mchana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa maeneo mengine ili kupunguza msongamano uliopo katika kambi ya Nyarugusu.

0 comments:

Post a Comment